KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday 27 March 2015

TABOA: SHERIA INABIDI ZIBADILISHWE

MWENYEKITI Wawamiliki wa Magari ya Abiria (Mabasi) Tanzania (TABOA), Ramadhan Mrutu, amesema matukio ya ajali mchini yanachangiwa na vyombo vya serikali kwa kushindwa kwao kusima sheria kikamilifu.

Mrutu alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na wandishi wa habari kuhusu matukio ya ajali yaliyotokea katika kipindi hiki cha Machi mwaka huu.

Alisema ajali hizo zimesababisha vifo vya watu wengi huku wengine wakibaki na vilema vya kudumu.

 Mrutu alisema ajali hzo zinachangiwa mambo manne au matano, kwanza polisi kushindwa kusimamia ratiba, Sumatra kujaza magari mengi kwenye barabara moja bila kufanya utafiti wa kuona kama yanatosha au la.

Kingine ni kinachochangia ajali hizo ni kwa  madereva kupenda kwenda mwendo wa kasi, wako baadhi ya wamiliki wanaopenda magari yao kuwa ya kwanza kule yanako kwenda.

Pia baadhi ya abiria nao wanachangia ajali hizo kwa kuwataka madereva wakimbie, wamekufikia hatua ya kuwaahidi madereva kwamba kila atakapopigwa toshi na polisi asiwe na wasiwasi watazilipia.

Mrutu alisema ili kukomesha matukio hayo lazima Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (Sumatra), kuangalia utaratibu wake wa kujaza magari katika barabara moja ili yaende sambamba na wingi wa abiria.

“Mfano Sumatra inapeleka magari zaidi 20 kutoka Dar es Salaam, yakiondoka saa 12:00, asubuhi kwenda  Mbeya hali hiyo inachangia magari mengi kutojaa abiri hivyo madereva kukimbizana njiani kwa ajili ya kugombea abiria, matokeo yake ni ajali,”alisema Mrutu.Mrutu, alisema kama Kikosi cha Usalama Barabarani kitafanya kazi kwa uadilifu anaamini kuwa ajali hizo zitapungua.

Alisema kwa vile polisi wameshindwa kufanya kazi zao vizuri wanapendekeza kikosi hicho kifanyiwe mabadiliko ili waje polisi wengine watakaofanyakazi kwa uadilifu na hatimaye kuokoa maisha ya Watanzani wanaokufa kutokana uzembe wa watu wacheche.

Alisema kama serikali itaamua kudhibiti ajali hizo, inaweza tena kwa kuwatumia polisi waliopo kwani wanatosha na wala sio kweli kama polisi waliyopo hawatoshi.

Mwenyekiti Wawamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam, Sabri Mabrouk, alisema adhabu zinazotolewa kwa madereva wanaosababisha ajali ni ndogo, hivyo basi alishauri ikitokea ajali ambayo itabainika kisheria kuwa chanzo ajali hiyo kimetokana na uzembe dereva ni vema akahukumiwa kifo.

Hata hivyo, Mbrouk, alisema Machi 31 mwaka huu kutakuwa na mkutano wa wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri katika ukumbi wa Karimjee, mawazo yake hayo atayawasilisha katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment