KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday 5 April 2015

ASKOFU GWAJIMA: LOWASSA NI RAFIKI YANGU WA SIKU NYINGI

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema hakuna mtu atakayeweza atakayeweza kuvunja urafiki wake na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Gwajima, alisema kuwa hakumfahamu Lowassa barabarani, kwani bali walifahamiana tangu mwaka 1996 alipokuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Mijini alikuwa wakishirikiana  katika mambo mengi.

Askofu Gwajima alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati wa ibada ya Pasaka kwenye viwanja vya Tanganyika Pakers, Kawe.

Alisema urafiki wake na Lowassa hauwezi kuvunjika hata kama kuna maneno yanayoendelea kutolewa na baadhi ya watu.

Askofu Gwajima, alisema kuna makundi ya watu wanawazungumzia na kuingiza masuala ya kisiasa kwenye urafiki wao, hata hivyo, alibainisha kama ni hivyo au sio hivyo, lakini wanapaswa kuelewa kuwa Lowassa ataendelea kuwa rafiki yake. 

No comments:

Post a Comment