KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday 26 April 2015

WADAU WA HAKI ZA BINADAMU WAMTAKA MWANASHERIA MKUU KUFANYA MAREKEBISHO YA SHRIA DHIDI YA UKATI WA ULBINO

WADAU mbalimbali wa haki za binadamu wamependekeza kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iandae muswada wa marekebisho ya Sheria  ya kudhibiti Uchawi ambayo itasaidia kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye Ualbino.
 Mapendekezo hayo yanalenga  kutoa ulinzi na huduma za afya kwa watu wote wenye Ualbino nchini.
 Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishono mwa wiki,  Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala, Bahame Nyanduga, alisema tume inatoa wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa mapendekezo haya yanatekezwa.
Alisema sheria hiyo inayohitaji kufanyiwa merekebisho kuwa ni Sura ya 18 hususan Kifungu cha 8(1), kinachompa Mkuu wa Wilaya mamlaka  ya kumhamisha mtu anahisiwa kuwa mchawi kwenda kuishi sehemu nyingine.
 Alisema inapendekezwa kuwa kifungu hicho kirekebishwe ili washukiwa hao washitakiwe mara baada ya Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi wake.
 “Kwa kushirikiana na wadau wengine, iandae muswada wa marekebisho ya Sheria ya Tiba Asilia na Mbadala ya Mwaka 2001 kwa kuangalia hususan maana ya dawa tiba mbadla na kufuta vifungu vinavyoruhusu matumizi ya viungo vya wanyama katika dawa tiba mbadala,”alisema Nyanduga.
 Nyanduga, alisema wadau hao wanaishauri Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ianishe masuala ya mashtaka dhidi yay a watuhumiwa wa makosa ya mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino na kuyapa kipaumbele katika kuyashughulikia.

“Idara ya Mahakama iharakishe usikiliza wa mashauri ya mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino na kutoa hukumu kwa wakati ili kulinda haki za kundi hilo,”alisema Nyanduga.

Aliongeza kuwa kusema kuwa Jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau wengine, lifanye uchunguzi na upelelezi wa kina kubaini mtandao wa wanaojihusisha na mauaji ya watu wenye ualbino wakiwemo waganga wa jadi, wanunuzi, wakataji na watumiaji wakuuu wa viungo vya watu hao wenye ualbino.


Aidha,  wadau hao wameiomba serikali kutenga fedha za kutosha kwa taasisi zake zinazohusika na mapambano ya kukomesha ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino.


No comments:

Post a Comment