KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday 5 May 2015

WATU WENYE UALBINO KUPATA MATIBABU BURE MISENYI


MKUU wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagera FaNkurlu,dhili   amewalipia gharama za matibabu watu wote wenye ulemavu wa ngozi (albino)  walioko  katika  wilaya  hiyo,  ili  kuwawezesha  kupata  matibabu  kwakipindi cha mwaka mzima kuanzia sasa.
Kadi kwa ajili  ya matibabu hayo zilikabidhiwa leo, mkuu huyo wa wilaya,wakati wa hafla fupi ya chakula cha pamoja na watu hao wenye ulemavu wa ngozi,iliyofanyika katika wilaya hiyo na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwamoviongozi wa dini.
Akizungumza katika hafla hiyo Nkurlu alisema kuwa, kadi hizo walizokabidhiwawatu hao, zitawawezesha kupatiwa matibabu bila kudaiwa kutoa malipo wao nawategemezi wao, katika vituo vya serikali vinavyotoa huduma za afya na vile vyabinafsi vilivyosajiliwa na mfuko wa afya ya jamii (CHF).
Alisema  kuwa,  mbali  na  kukabidhiwa  kadi  hizo,  tayari  amekwishafanyamazungumzo  na  uongozi  wa  kiwanda  cha  sukari  cha  Kagera,  ili  albino  wotewatakaofika  katika  kituo  cha  afya  kilichoko  kattika  kiwanda  hicho  wapatiwematibabu bure, na kuwa ombi lake limekubaliwa.
 Mbali na hilo pia mkuu huyo wa wilaya ametoa simu za mkononi kwa watu hao, ilikuwawezesha albino wasio na mawasiliano kutumia simu hizo kutoa taarifa, pindiwanapoona watu wanaowatilia mashaka katika maeneo yao,  ili  hatua za harakazichukuliwe kabla ya kutokea madhara makubwa zaidi.
“Naendelea kufanya mawasiliano na vyama vya watu wenye ulemavu wa ngozivya nje ya nchi, ili waweze kuwasaidia kupitia chama chenu, kupata vitu ambavyohavipatikani huku kwa urahisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo gharamakubwa, mfano mafuta ya kuimarisha ngozi” alisema.

Aidha Nkurlu alitumia fursa hiyo kupiga marufuku wakuu wa shule za msingi nasekondari  zilizoko  katika  wilaya  hiyo,  kuwafukuza  shule  watoto  wa  albino  nakuwa atakayekaidi agizo hilo atamchukulia hatua za kinidhamu.
 “Kimsingi albino ni watu ambao hawawezi kufanya kazi za kuzalisha mali kamailivyo kwa mtu ambaye siyo albino,  kwa hiyo uwezo wao kiuchumii ni  mdogo kutokana  na  kutokuwa  na  uwezo  wa  kuhimiri  mikikimikiki katika  shughulimbalimbali, hivyo wahahitaji kusaidiwa,” alisema.
Akizungumza  katika  hafla  hiyo,  mwenyekiti  wa  baraza  la  waislamu  Tanzania(Bakwata) wa wilaya hiyo alhaji Abubakari Rutashobya, alisema kuwa madharayote yanayowakumba albino yanatokana na watu kuhama kwa Mungu na kwendakatika masuala ya ushirikina.
“Viongozi wenzangu wa dini mbalimbali, tujitahidi kuwarudisha watu wetu kwaMungu, watu wafundishwe wajue kuwa Mungu ni mgawaji kila mtu anayeingiahapa duniani ameandikiwa riziki yake, hivyo sio busara kuua wenzetu kwa madaiya kupata utajiri” alisema alhaji Rutashobya.
 Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika hivi karibuni,  wilaya ya Missenyi inakisiwakuwa na watu wenye ulemavu wa ngozi 14.

No comments:

Post a Comment