MBUNGE wa Bumbuli January
Makamba, anatarajiwa leo mjini Dodoma kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya
wana-CCM ili aweze kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais katika Uchaguzi
Mkuu mwaka huu.
Makamba, ambaye ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia, juzi wakati akitangaza nia ya kuomba
ridhaa hiyo, alisema akichaguliwa kuwa Rais hataunda Serikali ya wakwapuaji na
wabinafsi.
Alisema ataunda serikali
yenye utu na inayowasikiliza na kuwajali watu, inatimiza wajibu wake bila
chembe ya uzembe wala ulegevu.
“Nitaunda serikali yenye
Mawaziri wasiozidi 18, amabayo haitakuwa na mtu hata mmoja anayetiliwa shaka
kuhusu uwezo na uwadilifu waka.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam leo, Makamba alisema baada ya kufanya tafakuri ya kina yya changamoto
za sasa, akabaini kuwa nchi inahitaji uongozi wa aina mpya na ndio maama
akaamua kuomba nafasi hiyo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema anaomba ridhaa hiyo
kwa vile anaelewa kiu ya Watanzania ya kutaka kupata uongozi mpya, wa zama za
sasa, unaotoa matumaini mapya yatakayozaa Tanzania Mpya.
Makamba, alisema anaiomba
nafasi hiyo akiwa anaelewa misingi iliyoijenga nchi hii ambayo ni haki, umoja,
amani, mshikamano na upendo miongoni mwa Watanzania na kwamba iko haja ya kuilinda misingi hiyo.
Aidha, alisema uongozi
utakaochaguliwa mwaka huu ndio utaamua mustakabali wan chi hii, baada ya miaka
50 ya uongozi wa kizazi kilichopita, sasa ni wakati wan chi kuongozwa na
viongozi wa aina mpya, wenye mtazamo mpya, fikra mpya, maarifa mapya na
majawabu mapya.
“Nimesimama hapa kuwahakikishia
kwamba nimefanya tafakuri ya kina na
za
muda mrefu kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Na niko tayari kutengeneza na kuongoza
timu madhubuti ya Watanzania
wazalendo na waadilifu
watakaounda Serikali itakayojenga kesho
njema,”alisema Makamba.
Makamba,
alisema baada ya kuchukua fomu hiyo ataanza safari ya kwenda kusaka wadhamini
maeneo mbalimbali nchini.
MWISHO
No comments:
Post a Comment