KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday 7 July 2015

MCHUNGAJI MTIKILA ATINGA MAHAMANI KUSHITAKI MAKADA SITA WA CCM

MWENYEKITI wa Democratic Party, (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anatarajia kutinga mahamani kukifungulia mashtaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na amakda wake sita, akidai wameanza kampeni za Uchaguzi Mkuu mapema.
Makada hao ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, na mstaafu Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe.
Wengine ni William Ngeleja, Waziri wa Chakula na Kilimo Stephen Wasira na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba, ambao wote hao waliwahi kupewa adhabu Februari 18 mwaka jana, kwa kosa la  kuanza harakati za kuwania nafasi ya urais.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji Mtikila, alisema kuwa suala la makada hao sio la kuliacha hivi, hivi, kwani linagusa maslahi ya nchi.
Alisema, amefikia hatu hiyo baada ya kujiridhisha kuwa wanaushahidi wa kutosha juu ya vitendo vya makada hao kwenda kinyume na sheria za uchaguzi.
Mchungaji Mtikila, alisema makada hao wamejiingiza kwenye vitendo vya matumizi makubwa ya fedha kwa kusafirisha watu kwenda maeneo mbalimbali huku watu hao wakilewa na kulala bure.
“Wanasheria wetu hivi sasa wanapinda migongo katika kukamilisha mchakato wa shauri hili n kwamba litakapokamilika wakati wowote kuanzia sasa tutawaita kuwaeleza kwamba linakwenda mahakamani.
“Baadhi ya watu wanatafuta utawala kwa sababu ni meno ya kumung’unya rasilimali za nchi hii,”alisema Mchungaji Mtikila.
Mchungaji Mtikila alisema kuwa hatua hiyo ya kukifikisha chama hicho pamoja na makada wake hazitaishia hapo bali watafanya hivyo hata katika vyama vingine pindi watakapobaini vimeingia kwenye vitendo vya matumizi ya fedha chafu katika upataji wa wagombea wake.

“Kumekuwa na umwagwaji kubwa wa mabilioni ya fedha chafu kwa ajili ya kusaka madaraka jambo ni sawa na uhalifu na uhani,”alisema Mchungaji Mtikila.

No comments:

Post a Comment