MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Damiani
Lubuva, amesema baada ya kubaini changamoto zinazoikabili kazi ya uboreshaji wa
daftari la mpiga kura kwa kutumia mfumo wa kieletroniki (BVR), tume inatarajia
kukutana na Wakurugenzi Halmashauri za jiji la Dar es Salaam.
Jaji Lubuva, alisema hayo wakati alipozungungunza na wandishi wa
habari kuhusu kazi hiyo ambayo inaendelea huku kukiwa na matatizo ambayo katika
vituo vingine yamesababisha wananchi kupigana.
Alisema lengo la kukutana na wakurugenzi hao ni kufanya tathimini ili
kubaini mafanikio na upungufu, kisha kutafuta ufumbuzi pale penye changamoto.
“Ingawa kuna matatizo ya machine hapa na pale bado tume yetu imeweza
kufanikiwa hadi sasa katika kazi hii, ni viombe vyombo vya habari mtusaidie
kufikisha taarifa sahihi baadala ya kuandika habari tofauti,”alisema Jaji
Lubuva.
Jaji Lubuva, alisema katika kuwaondolea kero wakazi wa jiji la hilo
NEC imefanikiwa kuongeza mashine na
kwamba hivi sasa ziko zaidi ya 6000.
Alisema kuwa NEC inajukumu la kuhakikisha kuwa hakuna mkazi wa jiji
hilo anajiandikisha katika daftari hilo, akibainisha kuwa haingekuwa rahisi
kusema kwamba tume itaongeza muda kwa vile muda haujaisha.
Jaji Lubuva, alitoa ufafanuzi wa uandikishaji katika wilaya za mkoa
hizo kwamba katika Wilaya ya Temeke waliojiandikisha ni 188936, Ilala ni 220865
na Kinondoni ni 178961.
“Katika wilaya ya Ilala kuna kata 36 vituo 396, Temeke kata 32 vituo
572 na Kinondoni ina kata 34 vituo 706 ukiangalia utaona vijana wetu wamefanya
kazi kwa uweledi pamoja na mashine hizo chache,”alisema Jaji Lubuva.
Akizungumzia, kuhusu wanafunzi kuwa huenda baadhi yao watakakosa haki
yao ya kikatiba ya kupiga kura, Jaji Lubuva, aliwaonya wanasiasa kuacha
kulifanya jambo hilo kuwa la kisiasa.
Naye Profesa Amon Chaligha, alitolea ufafanuzi suala hilo la
wanafunzi, akisema tume inautaratibu, kwamba kila inapokaribia siku za uchaguzi
hususan kuanzia Septemba, tume inatoa fursa kwa wananchi wote wakiwemo
wanafunzi wanaotaka kubadilisha taarifa zao kutoka sehemu ya awali
alikojiandikishia kwenda aliko.
“Naona manawazungumzia hao tu mbona hamwazungumzii wale ambao ndio
kwanza wamekwenda kuanza masomo kwa mara ya kwanza kwani hawa ndio wengi kuliko
hao mnaowasemea,”alisema Profesa Chaligha.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Salum Mwalim, alisema kuwa alipata bahati ya kuzungumza na Mkurugezi Mpya wa
NC, ambaye alimhakikishia kuwa atawachukulia hatua wale wote ambao utendaji una
mashaka.
Alisema mkurugenzi huyo alisema kuwa atawaondoa wale wote ambao
hawana ujuzi na hiyo, kwamba watatafutwa watu wenye utaalamu.
“Kwa kweli kwa muda wa siku mbili alizokaa katika ofisi hiyo ameonyesha
imani kubwa kwa wadau na ndio maana kwa siku hizo kunaongezeko la watu katika
uandikishaji huo,”alisema Mwalimu.
Aliwasihi wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuacha kuogopa foleni na
baadala yake wajitokeze kwa wingi katika vituo, kwa lengo la kutimiza azima yao
ya kuandikishwa.
Alisema watambue kuwa bila kujiandikisha hawatapata fursa ya kupiga kura
katika uchaguzi mkuu Oktoba kwaka huu.
No comments:
Post a Comment