Mkurugenzi Mtendaji, Charles Msonde |
JUMLA ya watahiniwa 38,853 sawa na asilimia 97 waliofanya
mtihani wa kidato cha sita (ACSEE), Mei mwaka huu wamefaulu.
Kati ya watahiniwa hao wasichana waliofaulu ni 11, 734 sawa
na asilimia 98 wakati wavulana ni 27, 119 sawa na asilimia 97.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjni Zanzibar, Katibu wa Baraza la
Mitihani ya Taifa (NECTA), Charlse Msonde alisema kuwa watahiniwa wa shule
waliofaulu ni 34, 777 sawa na asilimia 98 huku wasichana ni 10, 576 sawa na
asilimia 99 na wavulana ni 24, 201 sawa na asilimia 98.
Msonde alisema kuwa jumla ya watahiniwa 4, 076 wa
kujitegemea sawa na asilimia 88 wamefaulu mtihani huo.
“Kati ya watahiniwa
40.753 waliondikishwa kufanya mitihani
ya kidato cha sita wakiwemo wasichana 12,113 (29.72%) na wavulana 28.640 (70.28%)
kati ya watahiniwa waliosajiliwa na shule
walikuwa ni 35,375 na wa kujitegemea walikuwa 5,378, mwaka 2014
watahiniwa waliosajiliwa walikuwa ni 41,968 kati ya watahiniwa hao walifanya
mitihani ni 39,805 sawa na 97.67 na watahiniwa 948 sawa na asilimia 2.33 hawakufanya mitihani yao” alisema Msonde.
Msonde alisema takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa ufaulu
wa watahiniwa wa shule katika masomo ya Historia, Gographia, Kingereza,
Fizikia, Kemia, Balogia, Uchumi, Biashara pamoja na Akaunti umepanda
ikilinganishwa na mwaka 2014.
“Ufaulu wa juu kabisa ni ule wa masomo ya Kiswahili na
Historia ambapo asilimia 99 ya watahiniwa wote wa shule waliofanya masomo hayo
wamefaulu, aidha ufaulu katika masomo ya Sayansi umeendelea kuimarika
ikilinganishwa na ufaulu wa masomo hayo kwa mwaka jana,”alisema.
Hata hivyo Msonde alisema kuwa ubora wa ufaulu kwa
kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya
watahiniwa 31, 450 sawa na asilimia 89 wamefaulu katika madaraja ya
Distinction,Merit na Credit, wakiwemo wasichana 9, 876 na wavulana 21, 574.
Aidha alieleza kuwa jumla ya watahiniwa 40, 753
waliosajiliwa kufanya mtihani huo mei mwaka huu ni watahiniwa 39, 805 tu sawa
na asilimia 97 walifanya mtihani huku watahiniwa 948 sawa na asilimia 2 walishindwa kufanya
mtihani huo.
Shule
zilizofanya vizuri zaidi
Msonde alisema kuwa ubora wa shule umepangwa kwa kutumia
kigezo cha wastani wa pointi na upangaji wa shule hizo umezingatia shule zenye
idadi ya watahiniwa wasiopungua 30.
Alisema shule kumi bora ni Feza Boy’s (Dar es Salaam),
Runzewe (Geita), Feza Girl’s (Dar es Salaam), Sumbawanga (Rukwa), Ivumwe
(Geita), St Mary’s Mazinge juu (Tanga), Vwawa (Mbeya), Kisimiri (Arusha),
Namabengo (Ruvuma) pamoja na Scolastica (Kilimanjaro).
Shule
kumi za mwisho
Alisema kuwa shule kumi za mwisho ni Bariadi (Simiyu),
Ilongero (Singida), Lwangwa (Mbeya), Kilangalanga (Pwani), Kaliua (Tabora),
Logoba (Pwani), Iwalanje (Mbeya), Mtwara Technical (Mtwara), Kwiro (Morogoro)
pamoja na Meta (Mbeya).
Watahiniwa
waliofanya vizuri zaidi
Msonde alisema kuwa watahiniwa waliofanya vizuri zaidi
wamepatikana kwa kulinaganisha wastani wa pointi (GPA) kwenye masomo ya
tahasusi (Combination) pamoja na wastani wa alama za jumla walizopata.
Alisema kuwa watahiniwa hao ni Ramadhani Gembe (Feza
Boy’s), Lesian Lengare (Ilboru), Hunayza Mohamed (Feza Girl’s), Rosemary
Chengula (St Mary’s Mazinde juu), Kevin Rutahoile (St Joseph’s Cathedral),
Anderton Masanja (St Joseph’s Cathedral), Joseph Pasian (Iliboru), Lupyanal
Kinyamagoha (Mzumbe), Yonazi Senkondo (Feza boy’s) pamoja na Meghna Solanki
(Shaaban Robert).
Msonde alisema kuwa tathimini ya awali ya matokeo kwa
watahiniwa wa shule yamezidi kuimarika kwani ufaulu umepanda kwa asilimia 0.61
kutoka asilimia 98.26 mwaka 2014 hadi asilimia 98.87 kwa mwaka huu.
Alisema tathmini ya ufaulu wa shule mbalimbali inaonesha
kuwa katika shule kumi bora kitaifa shule za serikali ziko tano na zisizo za
serikali ziko tano, aidha alieleza katika shule ishirini bora kitaifa shule za
serikali ziko 13 na zisizo za serikali ni saba.
Alisema kuwa kuhimarika huko kwa ufaulu kwa mwaka huu
ikilinganishwa na mwaka jana ni matokeo ya juhudi zinazoendelea kufanywa na
serikali katika kuboresha elimu nchini.
Matokeo
yaliyozuiliwa
Alisema kuwa watahiniwa 10 wa shule ambao waliugua wakati
wa mtihani na kushindwa kufanya mitihani kwa baadhi ya masomo matokeo yao
yamezuiliwa.
“Watahiniwa hawa 10 na wengine 25 ambao awakufanya masomo
yote wamepewa fursa ya kufanya mitihani yao Mei, 2016,” alisema.
Matokeo
ya mtihani yaliyofutwa
Msonde alisema kuwa baraza limefuta matokeo yote ya
watahiniwa watano waliobainika kufanya udanganyifu.
Aidha Msonde alisema anazipongeza kamati za uendeshaji
mitihani za mikoa na wilaya, wakuu wa shule na wasimamizi kwa kuzingatia na
kusimamia ipasavyo taratibu za uendeshaji wa mithani hiyo.
“Nwapongeza sana imeweza kuzuia kwa kiasi kikubwa
udanganyifu lakini pia nawapongeza watahiniwa wote waliofanya vizuri na
kutojihusisha na udanganyifu,” alisema.
Matokeo
mengine yaliyotangazwa
Matokeo mengine ya mitihani yaliyotangazwa na katibu huyo ni Ualimu daraja la A, mtihani wa
Stashahada ya ualimu Sekondari, stashahada ya ualimu ufundi na ualimu daraja A
kozi maalum.
Watahiniwa walisajili kufanya mtihani daraja la A ni 14,106
sawa na asilimi 62 .81ya watahiniwa wote waliosajiliwa watahiniwa wa mtihani wa
ualimu ndaraja A kozi maalum 158 sawa na
asilimia 53.80 ya watahiniwa wote waliosajiliwa kati ya waliosajiliwa 155
walifanya mitihani huku watatu wakiwa hawakufanya mitihani hiyo.
Watahiniwa waliosajiliwa kufanya stashahada ya ualimu wa
Sekondari ni 4,788 kati ya walisajiliwa 4,765 walifanya mitihani yao watahiniwa
23 hawakufanya mitihani ,katika watahiniwa wa stashahada ya ufundi
waliosajiliwa walikuwa ni 4 watahiniwa
watatu walifanya mtihani na mmoja hakufanya .
No comments:
Post a Comment