Dk. Ave-Maria Semakafu |
VYAMA vya Siasa nchini vimetakiwa kuyajengea uwezo makundi
ya watia nia wa wanawake, watu wenye ulemavu na vijana ili yaweze kushiriki
katika mchakato wa chaguzi mbalimbali nchini.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa
Mtandao wa Jinsia (TGNP Mtandao), Grace Kisetu, wakati alipokuwa akitoa mrejesho
kwa viongozi wa vyama hivyo, uliyotokana na mafunzo kwa watia nia hao
yaliyofanyika hivi karibuni.
Alisema, hivyo kwa vile watia nia hao, wakati wa
mafunzo walieleza kwamba kila kinapofika
kipindi cha uchaguzi makundi hayo yamekuwa yakikabiliwa na matatizo ikiwemo
rushwa, upendeleo wa kidugu bila kujali uwezo wa wahusika.
“Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo makundi haya ili yaweze kuteuliwa ili wapate haki
katika vyama vyao, hatimae waweze kuingia katika uchaguzi,”alisema Grace.
Alisema, walianza kutoa mafunzo kwa wadau na jamii kwa
ujumla ili na yenyewe ione kuwa mwanamke akipewa uongozi anawaweza hivyo
aminike.
Hata hivyo mafanikio ya mafunzo hayo mafanikio yake
yataanza kuonekana katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2020.
Naye Mratibu wa Ulingo, Dk. Ave-Maria Semakafu, alisema
kuwa kumekuwa na matatizo ya kuwapata watia nia wakati wa mafunzo kutoka katika
vyama hivyo.
Alisema, hali hiyo imekuwa ikichangiwa vyama vyote vya
siasa nchini kutokuwa na mawasiliano kutoka ngazi ya chini hadi taifa.
Dk. Semakafu, alisema kutokana na mazingira hayo
aliwataka viongozi wa vyama hivyo kuanzisha daftari la kudumu la wanachama.
“Kumekuwa na ubabaishaji wakati wa kuwakuwakilisha majina
ya washiriki wa mafunzo kwani baadhi ya viongozi wamekuwa wakipeleka majina ya
ndugu zao au kuuza nafasi hizo, sasa hii inatia shaka,”alisema Dk. Semakafu.
Alisema kwa chama ambacho kina lengo la kuongoza
nchi kuanza kujiingiza katika vitendo
vya rushwa hiyo ni hatari na kwamba hakiwezi kuaminika tena katika jamii.
No comments:
Post a Comment