KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday 14 July 2015

WAKAZI WA JIMBO LA MBAGALA BADO HAWAJUI KATA ZAO RASMI



Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damiani Lubuva
BAADHI ya wakazi wa Kimara wilayani Ubungo jijini Dar es Salaa wamesema kuwa wameridhishwa na kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuligawa Jimbo ya la Ubungo na kuzaliwa Jimbo jipya la Kibamba.
Hata hivyo kwa ipande wa Jimbo jipya la Mbagala, lililoko katika Halmashauri ya Temeke wakazi wake pamoja na viongozi wamekuwa wagumu kuzungumzia hilo.
Akizungumza na wandishi jijini jana, kwaniaba ya wenzake, Ephraim Kinyafu, ambaye ni diwani anayemaliza muda wake, alisema wananchi hawana shida na ngawanyo huo bali hawa kuridhi na hatua za serikali kulifanya Jimbo la Ubungo kuwa Wilaya bali walitaka liwe Halimashauri.
Alisema, kuridhika kwao huko kunatokana na NEC kupokea maombi na mapendekezo ya kuanzisha jimbo la jingine la uchaguzi kutoka kwa wadau wa lillilokuwa Jimbo la Ubungo.
Aidha, alizitaja kata zilizoko katika Jimbo hilo kuwa ni Saranga, Goba, Mbezi, Kwembe, Msigani na Kibamba yenyewe.   “Ingawa wenzetu hawa wameligawa jimbo hili kwa dhamira mbaya inayolenga uchaguzi, ni wahakikishie kuwa tutashinda majimbo yote kwa maana ya Jimbo la Ubungo na lile jipya la Kibamba,”alisema Kinyafu.
Alisema, kugawanywa kwa jimbo hilo kutasaidia kuchechemua maendeleo ya kijamii katika jimbo jipya la Kibamba, kwa mfano, itabidi katika jimbolo jipya kujengwe hospitali kama ilivyo katika makimbo mapya.
Kwa upandea wa Jimbo la Mbagala mmoja wa viongozi ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema hadi sasa hawajui ni kata zipi zimekwenda kigamboni au nizipi zimechukuliwa kutoka Temeke.
Alisema, ingawa kuna taarifa kuwa mpaka ni wa jimbo la Mbagala na Kigamboni ni barabara kubwa, hata hivyo, anajiuliza kama ni hivyo jimbo hilo litakuwa dogo kwa sababu haamini kama Temeke itakubali kumegwa eneo lake.
Hata hivyo, kiongozi huyo, alisema kwa vile hawajaiona taarifa hiyo ya NEC, itawabidi wasubiri kuona mgawanyo wa kata hizo.
Jitiahada za wandishi ili kumpata  Ofisa Habari wa Halmashauri hiyo ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita muda mrefu bila kupokelewa.
Juzi Tume hiyo ya uchaguzi ilitangaza majimbo orodha ya majimbo mapya 26 ya uchaguzi Tanzania Bara kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka Huu.

No comments:

Post a Comment