KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday 29 July 2015

WAMACHINGA WALIOVAMIA JANGWANI KUONDOLEWA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
MKUU wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Issaya Mngurumi, wametoa siku mbili kwa wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga), waliovamia eneo la Jangwani kuwa hadi Jaulai 30 wawe wameondoka.
Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kuutaka uongozi wa Manispaa ya Ilala kusitisha zoezi la ugawaji wa eneo la Jangwani kwa wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga) kwa kuwa eneo hilo si salama.
Akizungumza na wandishi jijini Dar es Salaam jana, Mushi, alisema kuwa Manispa hiyo haijagawa eneo hilo kama inavyodaiwa wafanyabiashara hao.
Alisema, wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa eneo hilo limevamiwa na watu ambao hawakuwa lengo la manispaa hiyo kwani waliyotakiwa kwenda pale walikuwa ni wamachinga wanaotandika biashara zao chini katika eneo la Kariakoo.
Mushi, alisema baada ya siku mbili hizo kupita manispaa hiyo itatumia nguvu kuwaondoa katika eneo hilo tena bila kujali gharama walizoingia katika ujenzi huo.
“Ni vema wakazitumia siku hizi mbili kuboa mabanda yao ili kuepuka hasara ambayo inaweza kujitokeza baada ya muda uliyotolewa kupita,”alisema Mushi.
Mushi, ambaye baadhi ya wafanyabishara hao walidai kuwa alikuwa ni mmoja wa viongozi alitoa agizo la wao kwenda katika eneo hilo, alipinga vikali kuhusika katika mpango huo.
“Mimi sina maeneo mwenye maeneo ni Halmashauri ya Ilala kwa hiyo siana uwezo wa kugawa maeneo kama wanavyodai,”alisema Mushi.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mngurumi, aliwataka wafanyabiashara hao kutekeleza agizo haraka kabla muda haujapita kinyume chake atapeleka greda kwa ajili ya kuvunja mabanda yote.
“Kumetokea upotoshaji kwani wakati wanawapeleka wafanyabiashara hao wa Kariakoo tuliwaeleza wazi kuwa hawana ruhusa ya kujenga mabanda bali walikubaliana kuwa wataendesha biashara zao kwa kuzitandika chini,”alisema Mngurumi.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini juzi, Mwanasheria wa Baraza hilo, Manchare Suguta, alisema, wakiwa wasimamizi wa mazingira wamelazimika kuwaandikia uongozi wa manispa hiyo barua Julai 24 mwaka huu wakiwataka kusitisha uamuzi wao haraka.

No comments:

Post a Comment