CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimepata majimbo 19 baada ya kukamilika
majadiliano ya ugawaji wa majimbo kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Chama hicho kimepata majimbo hayo kati ya 265 ndani ya vyama
vinavyounda Ukawa ambavyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama
cha Wananchi (CUF), NLD na NCCR-Mageuzi.
Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Nderakindo Kessy . |
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu
Katibu Mkuu wa Uchaguzi, Mwalimu Nderakio Kessy, alisema majimbo hayo yamefikia
19 baada ya kukamilika majadiliano kuhusu majimbo 12 yaliyokuwa yamebaki kati
ya 265.
“Kama mnavyofahamu kwamba awali chama chetu katika mgawanyo kilipata
majimbo 14, lakini hivi sasa majimbo yetu yameongezeka kufikia hadi 19,”alisema
Aliyataja majimbo hayo ni Kasulu Vijijini na Mjini, Buyungu, Muhambwe,
Kigoma Kusini, Manyovu, Mwanga, Vunjo, Mtwara Mjini, Mufundi Kusini.
Mengine ni Gairo, Kibakwe, Mpwapwa, Mtera, Ngara, Mbinga Vijijini,
Ileje, Nkenge na Serengeti.
“Tumekubaliana kati ya majimbo 265 ya uchaguzi NCCR-Mageuzi
inasimamisha wagombea katika majimbo 19 kati ya majimbo hayo 265,”alisemaMwalimu
Nderakio.
Hata hivyo, Mwalimu Nderakio, alishindwa kuyataja majina ya wagombea
na majimbo yao kutkana na mchakato wa kukamilisha ujazaji wa fumu kutokamilika
kwa asilimia 100.
Alisema hadi sasa mchakato huo umekamilika kwa asilimia 86, huku kwa
wale ambao bado kukamilisha wanaendelea ili waweze kukamilisha na kutangazwa
majina hayo.
Aidha, alikanusha taarifa zilizochapichwa kwenye chombo kimoja cha
habari kuhusu kujitoa kwa chama hicho katika Ukawa na kusema kwamba hazina
ukweli wowote.
“Chama kina utaratibu wake kila kinapotaka kutoa taarif inafahamika
kuwa msemaji ni mwenyekiti, kwa aliyetoa taarifa hiyo chama kimebaini kuwa
aliyetoa hayuko Dar es Salaam,”alisema
Mwalimu Nderakio, alisema, msimamo wa chama hicho ni kutokujitoa katika
Ukawa na kuongeza kuwa kitakuwa cha mwisho kutoka.
Alisema lengo kuu la kuanzishwa umoja huo
ulitokana na yale yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Bunge la Katiba jambo ambalo
kwa zaidi ya miaka 20 chama hicho kilikuwa kikipigania kupatikana Katiba Mpya
kwa ajili ya ustawi wa
No comments:
Post a Comment