KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday 16 August 2015

SUMAYE: SIJUI WANAONIVUMISHIA MAMBO YA AJABU AJABU WANA NIA GANI

WAZIRI Mkuu wa zamani Frederick Sumaye, ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya watu kuvumisha kuwa jana angekutana na vyombo vya habari ili kutangaza kujivua uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Siku za hivi karibuni tangu kuhama kwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu Eduard Lowassa, kumezuka wimbi kubwa la baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM kujivua uanachama na kuhamia Chadema.
Akizungumza na wandishi, jijini Dar es Salaam leo, Sumaye, alisema taarifa hiyo ilimshangaza kwa avile hakuwa na mpango huo.
Alisema hivyo, kwa vile hakuwahi kuzungumza na mtu yeyeto na hajui chochote kuhusu mkutano huo na vyombo vya habari isitoshe hivi sasa yuko Hanang.
“Mimi watu ambao wameniuliza nimewambia yani hiyo kitu hata mimi sijui kiukweli wala siko Dar es Salaam ni hivi sasa niko Hanang.
“Ninasikia kuna mwandishi ameamua kutupia taarifa hiyo kwenye mambo yenu haya ajabu ajabu, hajazungumza na mimi wala sijawahi kuzungumza naye wala sina mpango huo,”alisema Sumaye.
Kuhusu kuhamia Chadema, Sumaye, alisema kama angekuwa na mpango wa kuhamia chama hicho angeviambia vyombo vya habari au angeonekana akipewa kadi.
“Hivi mimi naweza ni kamahama kisiri siri kweli ni waambie tu kuwa sina mpango wowote wa kukihama chama hiki,”alisema Sumaye.
Sumaye, aliwashangaa na haelewei wanaofanya hivyo wana lengo gani naye, akidai mbona hawaandiki taarifa za hao wanaohama, wange waandika hao kama wanataka kuandika.

No comments:

Post a Comment