KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday 2 August 2015

VYAMA VYA SIASA VYATAKIWA KUZIWEKA HADHARANI ILANI ZA UCHAGUZI MWAKA 2015/20

WAKATI zikiwa zimesalia siku 18 kuanza kampeni za urais, ubunge na udiwani, karibu vyama vyote havijatangaza Ilani zao kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Hayo yalisemwa na baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati walipozungumza na wandishi leo, kuhusu kuchelewa kutangazwa kwa Ilani hizo hadharani.
Amos Joseph ambye ni mwalimu na mwanaharakati wa kutetea makundi maalumu, alisema kuwa kuwekwa hadharani kwa Ilani hizo kutasaidia kujua ni jinsi vyama hivyo vilivyojipanga katika kuyasaidia makundi hayo.
“Unajua kunavipaumbele ambavyo tunapaswa kujua mapema mfano fursa za upatikanaji wa dawa kwa makundi ya wagonjwa wenye ukimwi sasa bila kuwekwa hadharani kila mmoja wetu akaipata kirahisi na kwamba ukiitaka lazima uiombe, itakuwa hawatutnei haki,”alisema Joseph.
Alisema ukiachilia mbali kundi hilo bado kuna makundi ya watu wenye ulemavu na wanawake na vijana haijajulikana Ialani hizo zinasema kuhusu ushiriki wao katika ngazi za maamuzi.
“Nimesikia baadhi ya watu wakisema vyama vyote vikubwa wameishazitoa lakini mbona hazionekani huku mitaani huu ni wakati wa uwazi hivyo tunataka zionekane kwa urahisi kila mmoja azisome,”alisema Joseph.
Ofisa habari wa Mtandao wa Jinsia (TGNP Mtandao), Deogratius Temba, alisema kuwa hadi sasa amefanikiwa kupata Ilani ya chama kimoja ambacho ni ACT-Wazalendo.
Alisema, kama vyama vinapaswa kuwapatia Ilani hizo ili wajue vinataka kuwafanyia nini wanachi vitakapopewa dhamana.
“Viongozi wa vyama tupeni Ilani zenu tujue mnataka kufanya nini mkipewa dhamana. na msikopy na kupeste zile za 2010,”alisema Temba.
Msemaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tumain Makene, alisema kuwa wanatarajia kuiweka hadharani 

Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa NCCR-Mageuzi Faustine Sungura, alisema kwa vile yao haijatumika wanatarajia kuitangaza hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment