Sheikh wa Jumuiya, Taasisi za Kiislam na Shura za Maimamu, Rajab Katimba |
BAADHI ya viongozi wa dini nchini wamelitaka Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), kuacha kuzuia wananchi katika kufuatilia wa
wakilishi wao bungeni kwani kunawanyima hivyo ni sawa na kuwanyima haki ya
kupata habari. Sheikh wa Jumuiya, Taasisi za Kiislam na Shura za Maimamu,
Rajab Katimb, alisema Jumuiya hiyo imesikitishwa na Kitendo hicho kwani kinakwenda
kinyume na mfumo wa kujenga demokrasia kwa kutumia vyombo vya habari.
Alisemam kuwa TBC halipaswi kuendeshwa kisiasa tena kwa
kudhani kuwa lipo kwa ajili ya Chama tawala baadala ya wananchi ambao ndiyo
wenye shirika hilo.
“Wanachofanya TBC pamoja na serikali yake hakikubaliki na
hakieleweki na kikubwa zaidi wanachofanya ni sawa na kufanya sensa ya taarifa
kisha watowe wanachotaka.
“Kama kweli wamezuia bunge kwa madai ya uchochezi hiyo siyo
kweli kwani kama nivitendo vya uchochezi basi kwa kiasi kikubwa chama tawala
kimehusika kwa kiasi kikubwa mfano ni Zanzibar wakati wa sherehe za Mapinduzi
baadhi ya wafuasi walipita mbele ya viongozi yaliyokuwa na maneno ya kibaguzi
ambayo yanaleta uchochezi,”alisema Sheikh Katimba.
Sheikh Katimba, alisema hakuna haja kwa vyombo vya habari
kudhibitiwa kwa vile vyombo hivyo hivi sasa vinachikua nafasi kubwa katika
kukomaza demokrasia kwa hiyo serikali haina haja ya kuwanyima watanzana uhuru
wakupata taarifa.
Alisema kuna haja kwa serikali kutoa uhuru kwa vyombo vya
habari ili viweze kuwahabarisha wananchi baadala ya kuvikatisha tama vyombo
hivyo mfano mzuri ni kufutwa kwa gazeti la MAWIO.
Naye Askofu wa Kanisa la Kipentekosti William Mwamalanga,
umoja wao unalaani kitendo kilichofanywa na wizara husika kwani kimeonyesha
wazi kutojali haki ya wananchi ya kupata habari.
Alisema TBC ni shirika la Watanzania ambalo kwa kiasi
kikubwa bdiyo sikio lao la kuwafikishia taarifa mbalimbali hususan zinazotokea
hivi sasa bungeni.
Akofu Mwamalanga, alisema kuwa kama TBC imeshindwa kutoa
huduma ni vema likatoa haki hiyo, kwa vyombo vingine vya habari kupewa nafasi
ya kuwafikishia wananchi habari hizo za Bunge ambazo ni muhimu sana kwa
wananchi.
“Shirika hili ni letu sote tena linaendeshwa kwa kodi za
Watanzania kwa hiyo kitendo cha kuzuia taarifa ni sawa na kuwafanyia dhuluma
walipa kodi wake,”alisema Mwamalanga.
Kwa upande wake James Watondoha, ambaye ni mkazi wa Mbezi,
alisema pamoja na kusikitishwa na kitendo cha kuzuiwa taarifa hizo za kibunge
lakini bado hakuridhishwa na mwanzo wa Bunge hilo.
Alisema, kuwa alitarajia kuwaona wabunge hao wakijikita
zaidi katika kupigania matatizo ya wananchi baadala yake wabunge hao walijikita
zaidi kwenye kutunishiana misuri jambo ambalo halitawasaidia Watanzania.
Watondoha, alisema kuwa kama wabunge hawataacha itikadi za
vyama vyao katika kujadili shida za wananchi kuna hatari Bunge hilo
likamalizika bila ya mijadala yeote kutopatiwa ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment