NAIBU WAZIRI, ANTHON MAVUNDE |
NAIBU
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na walemavu mheshimiwa Anthony Mavunde, amesema baadhi ya waajiri
ambao hawataki kutoa mikataba kwa mujibu wa sheria za kazi kiama chao kimekaribia.
Aliyasema
hayo baada ya kubaini ukiukwaji wa sheria za kazi katika kampuni mbalimbali za
watu binafsi kumekuwa chanzo cha misuguano kati ya waajiri na wafanyakazi
sehemu za kazi.
Akizungumza
kwenye kipindi cha Dakika 45; kinachorushwa na ITV kila Jumatatu kuanzia
saa 3 usiku, Mavunde, alisema serikali imechoshwa na misuguano hiyo inayotokana
na waajiri kupuuza madai ya wafanyakazi wao wanaodai mkataba wa ajira.
Alisema,
ili kuwabana waajiri hao, wasiyopenda kufuata sheria za kazi serikali imeamua
kuziangalia upya sheria hizo, kwa ajiri ya kuzifanyia marekebisho ambayo
yataweza kutoa adhabu kali ya papo kwa papo kwa mwaajiri yeyote ambaye atakaidi
kutoa mkataba kwa mfanyakazi.
“Niliwahi kufanya ziara za uguzi katika kampuni anbazo
siwezi kuzitaja kwa kweli nilibaini kuwepo kwa mambo ambayo ni kinyume na
sheria za kazi na yanafanyika kwa vile
mhusikaanajua anaweza kupigwa faini kisha akaendeleanautaratibu huohuo mbovu,”alisema
Mavunde.
Alisema, anaamini kuwa utaratibu huo wa adhabu kali unaweza
kuwa suluhisho ukilinganisha na huu wa sasa wa kufikishana kufunguliana kesi
kwenye mahaka ya kazi.
Mavunde, alisema licha ya mpango kuandaliwa lakini
bado Wizara yake inawataka waajiri wote kuwapa
wafanyakazi wao mikataba na kuwaruhusu kujiunga na mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja
na kuruhusu kufunguliwa matawi ya vyama vya wafanyakazi katika ofisi zao.
“Unajua kitendo cha kuwanyima mkataba wafanyakazi kuna
wanyima haki ya kuwekewa akiba katika mifuko hiyo ya kijamii pia wanaikosesha
serikali kodi sasa tunawataka wabadilike kwani siyo kila kitu lazima waelekezwe
na serikali kwani mbona sheria za kazi ziko wazi,”alisema Mavunde.
Mavunde, alisema nia yake kubwa ni kuona Sheria ya Kazi inafuatwa na waajiri
wote ili kujenga Tanzania ambayo itakuwa haina misuguano baina ya wafanyakazi
na waajiri jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo kwa kasi iliyoanzishwa na
Serikali ya Awamu ya Tano.
No comments:
Post a Comment