SPIKA wa Bunge Job Ndugai ametakiwa kuweka hadharani majina
ya wabunge, aliyodai kuwa wamekuwa wakiingia bungeni huku wakiwa wametumia
kilevi.
Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya Rais John Magufuli
kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga, anayedaiwa kuwa alionekana amelewa muda wa kazi pale alipokuwa
akijibu maswali ya wabunge katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana
Mwenyekiti wa Jukwaa la Watetezi wa Rasilimali wasiokuwa na Mipaka (WARAMI),
John Marwa, alisema wanampongeza Rais kwa hatua aliyochukuwa dhidi ya waziri
huyo kwa vile itakuwa fundisho kwenye jamii iliyozoea kuishi maisha ya mazoea.
Alisema wamefikia hatua hiyo, kutokana na kiongozi huyo wa
Bunge kukiri akiwa bungeni kwamba kuna wabunge wanakuwa wa,elewa hata kuvuta
bangi wakati wa mikutano ya Bunge ikiendelea hali iliyowafanya wananchi
kupoteza imani na chombo hicho muhimu.
“Kwa sababu Bunge ni chombo ambacho kinasemea wananchi
dhidi ya Serikali na kama kiongozi wa Bunge amekiri jambo hili tunamtaka aweke
wazi majina ya hao Wabunge hadharani ili chombo hicho cha uwakilishi kirudishe
heshima yake kwa Umma.
“Pia tunaomba sheria kali zitungwe ili kukidhi na kutoa
adhabu kali kwa Wabunge watakaobainika kujihusisha vitendo hivyo vya aibu wa
wapo ndani Bunge,”alisema Marwa.
Aidh, Marwa alisema endapo kiongozi huyo atashindwa kutaja
majina ya wabunge hao, basi watamtaka awaombe radhi wabunge na Watanzania ili
waendelee kuwa na imani na wabunge wao.
“Hatuwezi kusema
tutamchukulia hatua gani endapo atashindwa kufanya hivyo, cha msingi hapa ni suala la tunasubiri muda,”alisema
Marwa.
Katika
hatua nyingine Mkurugenzi wa Jukwaa la Watetezi wa Rasilimali
wasiokuwa na Mipaka WARAMI, Evance Kamenge, alimelitaka Jeshi la Polisi Kitengo
cha Usalama Barabarani (Trafic), kupitia upya sheria ya barabara za Mabasi ya
endayo haraka, ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa yale ni magari na siyo treni.
“Waifahamishe Kampuni ya UDRT kwamba, lazima waajiri
madereva wenye sifa za kuendesha magari ya abiria, pili madereva watambue kuwa wanaendesha magari
siyo treni.
“Kwa kuwa huu ni usafiri mpya WARAMI tunapendakeza
Mwekezaji wa mradi huu ahakikishe anatoa ajira kwa madereva wenye sifa stahiki
na wanaojua vema sheria za barabarani
kwani tumebaini wapo baadhi ya madereva ambao wamejenga kiburi kwa
kuitumia vibaya sheria ya mbasi hay,”alisema Kamenge.
Aidha, Kamenge, WARAMI, inamtaka mwekezaji kuangalia
uimarishaji wa vitoa ishara au honi kwa mabasi yake upya kwani hadi sasa
havijakuwa msaada wa kuepusha ajali katika makutano ya barabara.
Alisema tangu kuanza mradi huo takribani wiki mbili sasa
tayari kuna kumeripotiwa vifo vya watu watano waliyofariki kwa ajali
zilizotokana na uzembe wa madereva wa mabasi hayo au watumiaji wa barabara
hizo.
Kamenge, alisema wakati mwingene watumiaji wa barabara
hizo, wamekumbwa na ajali hizo kutokana na kutoelewa matumizi ya barabara hizo
kwani baadhi yao wamekuwa wakiingia kwenye njia hizo hali inayosababisha
wagongwe.
Pia, alisema WARAMI inapendekeza Kamati ya Usafirishaji
pamoja na Mkuu wa Mkoa kukaa chini upya kutafakari matumizi ya barabara hiyo
hususan kwa wavukao kwa miguu.
No comments:
Post a Comment