WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,
amesema Serikali itaweka mazingira wezeshi ili kuwawezesha Makandarasi wazawa
kupata miradi mingi ya ujenzi wa miundombinuya nchini.
Akifunga mkutano wa siku mbili wa Makandarasi Prof.
Mbarawa amesema, Serikali itatenga miradi mikubwa maalum kwa ajili ya Makandarasi
wazawa ili kuwajengea uwezo.
“Kazi yenu ni moja tu ni kuwajengea watanzania miundombinu
iliyobora ili wa/kie uchumi wa kati i/kapo 2025”, amesema Prof. Mbarawa.
Amesisitiza umuhimu wa Makandarasi wazawa kuungana ili waweze
kupata miradi mingi ya Serikali na kuijenga kwa muda sahihi kwa thamani
inayowiana na fedha wanazolipwa.
Amezitaka Taaasisi za fedha nchini zipunguze riba za
mikopo kwa Makandarasi wazawa ili kuwawezesha kukua na hivyo kupata miradi
mingi ya ujenzi ndani na nje ya nchi.
“Changamkieni fursa katika ujenzi wa bomba la mafuta kutoka
Tanga-Tanzania hadi Hoima- Uganda (km 1410), ujenzi wa reli ya kati na ujenzi
wa viwanda vikubwa vya kati na vidogo”,amesisitiza Prof. Mbarawa.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph
Nyamhamga, amewataka Makandarasi kujipanga vizuri kutumia fursa zilizopo katika
bajeti ijayo kwa kujenga miradi kwa ubora na gharama sahihi.
Amewaonya Makandarasi kuacha kufanya kazi chini ya
kiwango na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani husababisha miradi kutokuwa
na ubora uliokusudiwa.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Mhandisi
Consolata Ngimbwa amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Makandarasi wazawa wataungana
katika kutekeleza miradi mikubwa na kuiomba Serikali watengeneze mazingira ya Makandarasi wazawa kushirikiana na Makandarasi wa nje
katika ujenzi wa miradi mikubwa.
Asilimia 46 ya Bajeti ya Maendeleo ya mwaka 2016/2017 imetengwa
kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya miundombinu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment