MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI (IGP), ERNEST MANGU |
WATU 11 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro wakidaiwa
kumbaka binti wa miaka 21(jina linahifadhiwa).
Wakati huo huo, Mtandao wa Jinsia (TGN), unavitaka vvyombo
vya dola kuchukuwa hatua za haraka kuhakikisha watuhumiwa hao kesi yao
inaendeshwa kikamimilifu naa uminifu ili haki itendeke na iwe findisho kwa watu
wenye tabia kama hizo.
Akizungumza na wandishi kwa njia ya simu jana, Kamanda wa
Polisi mkoani Morogoro, Urlich Matei, alisema tukio hilo limetokea Aprili 28
mwaka huu kwenye nyumba ya kulala wawageni itwayo Titii iliyoko Dakawa wilayani
Mvomero.
“Chanzo cha tukio hilo ni kwamba binti huyo alikuwa na
mahusiano ya kimapenzi na Thabit,”alisema Matei.
Alisema alikumbwa na binti huyo alikumbwa ba mkasa huo baada
alipigiwa simu na Zuber Thabit (30) mkazi wa Mbarali Mbeya, akimtaka aende
katika nyumba hiyo ya kulala wageni, hata hivyo wakiwa chumbani aliingia Iddy
(32) Adamu mkazi wa Makambako, huku akiwa na kisu mkononi.
“Adamu alimtaka binti huyo asipige kelele na kumtaka afanye
kila atakachomuelekeza ndipo alipo walipotekeleza ukatili huo na kumtisha kuwa
asitoe siri hiyo vinginevyo atauawa,”alisema Kamanda Matei.
Alisema wakati Iddy akimtisha kwa kisu Thabit ambaye kazi yake ni dereva aliendelea kumbaka
na kumdhalilisha binti huyo.
“Wakati Thabit akiendelea Iddy alikuwa akiendelea kurikodi
picha za video kupitia simu yake kisha baadae kuzituma picha hizo kwenye simu
kwa njia ya Whatsapp kwa mtu aitwaye Rajabu Salehe (26), mkazi wa Dakawa,”alisema.
Matei, alisema baada ya Salehe kuzipokea naye alizisambaza
kwa picha hizo katika mitandao mbalimbali.
Aidha, Kamanda Matei, alisema baada ya tukio hilo la kikatili
kuripotiwa Kituo cha Polisi Dakawa Mei 4 mwaka huu, uchunguzi ulianza mara moja,
kisha kufanukiwa kukamata watuhumiwa hao 11 wakiwemo wabakaji hao na
waliyozisambaza tisa kati ya hoa 11.
Aliwataja watuhumiwa hao wengine tisa kuwa ni Rajabu Salehe
(26), Said Othman ((26), Musini Ngai (36), Said Mohamed (24), John Peter (24),.
Wengene ni Hassan Ramadhan (27), Ramadhan Ally (26) na Lulu
Peter (38), Magreth Njonjo (30), wote wakazi wa Dakawa.
Kamanda Matei, alisema watuhumiwa hao wamefunguliwa kosa la
kusambaza picha za utupu chini ya kifungu cha 14 (1) (a) cha Sheria ya Makosa
ya Mtandao.
Aliongeza kwa kusema kuwa jitihada za kuwatafuta watuhumiwa
wengine zinaendelea.
Aidha, jeshi la polisi mkoani humo linatoa onyo kwa wananchi
wote kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kutoshiriki makosa
kwani sheria ipo na inafanyakazi ipasavyo.
Mkurugezi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, alisema,wanalaani
tukio hilo la ukatili wa kijinsia kwani kitendeka ni udhalilishaji mkubwa na
unyama.
Alisema unyama aliyofanyiwa mwanamke huyo, ni kinyume na
sheria maalum ya makosa ya kujiamihiana (SOPA) ya mwaka 1998.
“Tunataka Watanzania
kuacha mara moja kusambaza video au picha za udhalilishaji wa wanawake, watoto,
wazee au makundi yiyote ambazo zinaonesha faragha au kuwadhalilisha kwa namna
yeyote kwani ni kinyume na sheria na Katiba ya nchi,”alisema Lilian.
Lilian, alisema serikali imeridhia mikataba na matamko mengi kuhusu haki za wanawake na usawa wa
kijinsia mfano mkataba wa kutokomeza aina zote za ukatili na dhuluma dhidi ya
wanawake na watoto (CEDAW) pamoja Mkataba wa haki za watoto (CRC).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee,
Ummy Mwalimu baada ya kuiona kwenye mitandao video hiyo, alikemea kwa mhuvu na
kusema huo ni udhalilishaji wa hali ya juu na hauvumiliki.
“Nakemea kwa nguvu zangu zote waliofanya kitendo hiki. Ni
unyama uliopitiliza. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu. Hatuwezi kuuvumilia.
Nimeshamuomba Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP wachukue hatua
stahiki haraka.
Pia nawaomba sana ndugu zangu msiesambaze hizo video. Hiyo ni
kuendelea kumdhalilisha huyo dada. Amebakwa na pia wamerekodi hilo tukio! Hii
haistahimiliki na haivumiliki. Mwalimu aliwataka wanawake wote na wanaume
wapenda haki na maendeleo ya wanawake kukemea kwa nguvu zote unyama huo.
No comments:
Post a Comment