KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday 25 October 2017

WAKAZI UTETE WALILIA MIKUTANO

WAKAZI wa Kitongoji cha Nyanda Katundu Kata ya Chemchem iliyoko katika Hamashauri ya Mji Mdogo Utete mkoani Pwani wamelalamikia kitendo cha viongozi kushindwa kuitisha mikutano ya vitongoji, kujadili maendeleo kwa muda wa mwaka mmoja sasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakazi hao kukabiliwa na kero mbalimbali ikiwemo wakulima kushindwa kujua wapi watakwenda kuuza mazao yao baada ya kukosa masoko.

Akizungumza katika Ofisi za gazeti hili jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho cha Nyanda Katundu, Omari Ngatima, alisema hafahu sababu has a inayo kwamisha vikao hivyo ambavyo ni mhuhimu kwa maenelo ya wananchi.

"Wananchi wanahitaji mikutano ya wenyeviti wa vitongoji ifanyika kwani wanaamini kuwa hao ndiyo wawakilishi waatakaofikisha kero za kwenye vikao vya ngazi ya juu ili ziweze kupatiwa ufumbuzi,"aliasema Ngatima.

Alisema, wakazi hao hao wanahitaji mikutano ya viongozi hao, kwani wanaamini kufanyika kwake ndiyo kutakuwa suluhu ya kumaliza matatizo yao yanayo wakabili hivi sasa.

"Kukosekana kwa vikao hivyo ambavyo vinatakiwa kufanyika maranne kwa mwaka kunarudisha nyuma maendeleo ya vitongoji vyote vilivyoko katika Kata zote tatu ambazo ni Chemchem, Utete na Ngalambe,"alisema Ngatima.

Ngatima, alisema kutokana na kukosekana na vikao hivyo, vitongoji hivyo vimeshindwa kujiletea maendeleo pia kudhibiti makusanyo ya kodi inayotokana na afanyabiashara wanaofika katika huko kukusanya mazao mbalimbali ikiwemo matikiti maji.

Aliongeza kuwa kukosekana na mikutano hiyo kunasababisha wananchi kushindwa kujua bajeti inayotengwa kwa ajili ya maendeleo ya jamii katika vitongoji hivyo.

Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Utete, Said Nassoro, akitolea ufafanuzi kuhusu madai hayo, alisema sababu kubwa zilozokwamisha vikao hivyo, zianafahamika na kila mmoja.

Alisema sababu kubwa ambazo zimekwamisha mikutano hiyo na usazalishaji mali katika maeneo ya Rufiji, Kibiti na Mkuranga ni kutokana na kukosekana usalama wa kuaminika kwa viongozi wa vijiji, vitongoji na wananchi.

Nassoro, alisema viongozi wa serikali na wale wa vyama vya siasa waliacha kuitisha mikutano hiyo kutokana na mauaji ya baadhi ya viongozi yaliyotekelezwa na watu wasiyojulikana.


"Hao wananchi wanasema tu, unaona wenzako wanakufa halafu unataka na mimi niitishe mkutano kwa kweli kwa hilo hakuna atakayekuwa tayari kwa ujumla viongozi wote katika maeneo hayo hawakuwa salama hali iliyowafanya wakimbie makazi yao,"alisema Nassoro.

No comments:

Post a Comment