KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday, 24 February 2015

WAKATI tukiuanza mwaka 2015 ni vema kwa wale tuliyoteuliwa tena kumshukuru mwaenyezi mungu wa rehema.

Pia tuwaombee wale waliotangulia mungu akaziweke  roho zao mahali panapostahili kwa vile yeye ndio mwenyekujua udhaifu wetu.
Nataraji kuwa mwaka uliopita tulishirikiana vizuri katika kuhabarishana hivyo nivema mwaka huu wa 2015 ushirikiano ukazidi kupita ule wa awali.

Pamoja na kuukaribisha mwaka mpya bado watu wenye ulemavu changamoto zao baadhi yake hazijapatiwa ufumbuzi hivyo ni vema kila mmoja wetu mwaka huu aongeze jitihada zaidi katika kuwatatulia changamoto hizo.
Niwaombe watunga sera katika mwaka huu wajaribu kuja na mbinu mpya ambazo zitasaidia kuwakomboa watu hao kutoka katika unyonge unaokabili.

Licha ya nasaha hizo leo Safu hii imepata bahati ya kutembelewa na Paulo Ezekiel, ambaye ni mkazi wa wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kijana huyu ni mlemavu wa miguu ambao ameupata hivi karibuni baada ya kuugua miguu kwa kipindi  cha zaidi ya mwaka kuanzia mishoni mwa mwaka 2013.

Kijana huyo anasema mwanzo wa aliingia Dar es Salaam mwaka 2011, akiwa katika shughuli zake maeneo ya Kariakoo alianguka ghafla na kupoteza fahamu ndipo alipookotwa na polisi na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa kuwa hakuwa na fahamu alipatiwa matibabu ya msaada kutoka hospitali hadi aliporejewa na fahamu alijikuta miguu yake haina uwezao wa kutembea tena.

mwanzo ilianza kupata ganzi kwa muda wa miezi mitatu huku akishindwa kutembea matokeo yakemwaka 2014  akapelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikaa kwa muda wa miezi minne.

Baada yauchunguzi wa madaktari Ezekiel aligundulika kuwa mishipa ya miguu yake imepoteza nguvu hali iliyomfanya ashindwe kutembea kama awali.
Kuanzia hapo akaanza kutembea kwa kutumia magongo huku pia akipewa ushauri wa kufanya mazoezi.

Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Ezekiel alikuwa akifanya kazi ya kuongoza wageni wanaotoka nje ya nchi hapa jijini Dar es Salaam.
Ni kijana mwenye uwezo wa kuzungumza lugha ya kingereza kwa ufasaha na ndio maana amekuwa akifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa.

Hata hivyo, tangu akumbwe na maradhi hayo hana uwezo tena wa kufanya kazi hali inayomfanya aishi maisha ya kubahatisha.
Kutokana na mazingira hayo anahitaji msaada kutoka kwa wasmalia wema na kikubwa anachohitaji ni msaada wa baiskeli ambayo anaamini kuwa itamsaidia kufanyia kazi zake na kujipatia kipato.

Ezekiel ni kijana ambaye anasema hapendi kuomba kwa vile anaona kitendo cha kuomba ni aibu hivyo akipata baiskeli hiyo atajiepusha na tendo hilo la kuomba.

Pia kwa dhati anawaomba kwa dhati msaada huo wa baiskeli kwani hawezi kupita mitaani na kuombaomba hali ya kuwa hana uwezo wa kutembea hivyo nawaomba wasmalia wema myaokoe maisha yake.

Labda katika hili ni Vema Watanzania wenye guswa na tatizo la kijana Ezekiel tujitokeze ili tuweze kumsaidia na amini wapo baadhi ya wadau wenye uwezo basi ni wakati wao wakujitolea na si kusubiri kutoa misada kwenye maeneo ambayo wanajua kuwa watapata faida.
Msaada wa kweli anapewa mtu asiyejiweza hivyo basi kuanzia sasa tujaribu kujenga utaratibu huo.


No comments:

Post a Comment