KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam FC Joseph Omog na
Msaidizi wake Ibrahim Shikanda, wametimuliwa rasmi kuinoa timu hiyo kutokana na
kushindwa kutimiza matakwa ya mkataba wao.
Akizungumza na Jijini Dar es Salaam leo, Mtendaji
Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba alisema, wamefikia hatua hiyo ya kumtimua Omog
Raia wa Cameroon na Shikanda Raia wa Kenya kutokana na kukiuka kipengele cha
mkataba wao.
Kawemba alikitaja kipengele hicho kuwa ni
kushindwa kuipeleka timu hiyo katika hatua ya makundi ya michuano ya Kimataifa
ambapo Azam FC ambao ni Mabingwa watetezi waliondolewa na El Merreikh kwa
kubugizwa mabao 3-2 baada ya nyumbani kushinda 2-0 huku ugenini wakichapwa bira
huruma 3-0.
“Katika makubaliano ya mkataba wetu na kocha
huyo na mwenzake kuna kipengere cha kuipeleka timu hatua za mbele zaidi kuanzia
makundi lakini cha kushangaza timu haijafanya hivyo, basi tumeamua kuachana nao
Omog na Shikanda,”alisema na kuongeza kuwa timu hiyo itaendelea kunolewa na
kocha msaidizi George Nsimbe mpaka kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hata hivyo habari za ndani ambazo Blog ilizipata
jana kutoka ndani ya klabu hiyo aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba Patric Liewig
anatajwa kurith mikoba ya Mcameroon huyo ambaye alichukua kijiti cha Stewart
Hall.
No comments:
Post a Comment