RAIS wa Mahakama ya
Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za watu Mhe Agustino Stephen Ramadhan
amesema kuwa hakuna haki ya mtu kukataa kutii Sheria na kuwataka
wananchi kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mikononi mwao .
Amesema kuwa katika
nchi yenye misingi ya Utawala Bora jamii inapaswa kuiachia mahakama
kutoa tamko juu ya mambo ambayo yanakinzana na jamii kwa lengo la
kuhakikisha kwamba jamii inapata haki kwa mujibu wa sheria .
Akizungumza kwenye
mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo Zanzibar
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ZSSF nje kidogo ya Mji wa Chake Chake ,
amesema kuwa mahakama ndio chombo ambacho kinatafsiri sheria na kutoa
haki .
Rais huyo ambaye pia
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Tanzania ametumia fursa hiyo kuwataka
wasaidizi wa Sheria kuwahudumia wananchi wanyonge kuweza kupata haki zao
na kujiepusha kutumia elimu waliyoipata kwa maslahi yao binafsi .
“Hakuna uhuru wa mtu
kukataa kutii sheria , hivyo jamii mnakiwa kutojichukulia sheria
mikononi mwao bali waiache mahakama kutoa tamko juu ya masuala
yanayoikinza jamii kwa lengo la kulinda amani ” alisisitiza .
Aidha amepongeza
juhudi zinazochcukuliwa na kituo cha sheria Zanzibar kwani kimeweza
kuleta mawimbi ya matumaini kwa jamii na kubomoa ukuta wa maovu ,
wanyinge pamoja na maonevu wanayofanyiwa wananchi hasa maskini.
Amefahamisha kwamba
katika misingi ya demokrasia na utawala sheria uhuru wa maoni ya
wananchi unazingatiwa na kuongeza kwamba taasisi binafsi zinaweza
kuchangia kuongezeka kwa uhuru wa wananchi .
“Kituo cha huduma za
sheria Zanzibar imekuwa ni moja ya taasisi ambazo zinachangia kukua kwa
uhuru wa maoni wa wananchi hasa katika nchi zinazofuata utawala wa
Sheria ” aliongeza Jaji Agustino Ramadhan .
Naye Mwenyekiti wa
Bodi ya wadhamini wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar Pr Chris Maina
Pita amesema kuwa kituo hicho kimekuwa mstari wa mbele kuwaelimisha
wananchi elimu ya Sheria ili waweze kuisaidia jamii yao inayowazunguka .
Amesema kuwa kituo
hicho kimeanda motisha kwa wasaidizi wa sheria wanaofanya vizuri katika
masomo yao na ambao wanataka kujiendeleza zaidi kusoma Elimu wa Sheria
kwamba kinadhamini gharama za masomo wa wanafunzi hao katika chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali .
“Kituo kimeandaa mfuko
kwa ajili ya wanasaidizi wa Sheria ambao wanataka kujiendeleza zaidi
kielimu katika vyuo vikuu , chuo kinagharamia gharama za masomo kwa
wanafunzi hao , na tayari wafadhili wameanza kuingi a fedha katika mfuko
huo ” alifahamisha .
Mapema Mkurugenzi
Mtendaji wa kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Harusi Miraji Mpatani
amesema kuwa tayari kituo hicho kimetoa wasaidizi wa Sheria 197 huku
wengine 82 wakiwa wanaendelea na masomo yao .
Mpatani ameeleza kuwa
kituo kinaridhiwa na utendaji wa kazi wa wasaidizi hao wa Sheria wa
Majimbo Zanzibar kwani wameweza kusaidia wananchi kupata haki .

No comments:
Post a Comment