![]() |
| WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi |
NA STEVEN WILLIAM
MKINGA
MGOGORO mkubwa wa ardhi umeibuka katika kijiji cha Segoma kata ya Mhinduro wilayani Mkinga mkoani Tanga kati ya wananchi wakijiji hicho na Wakala wa Misitu Tanzania ( TFS) ambao wapo chini ya serikali huku wananchi wakitishia kutoipigia kura CCM uchaguzi mkuu wala katiba pendekezi.
Mgogoro huo umeibuka baada ya wananchi wa kijiji hicho kudai kwamba mashamba yao ya asili na msitu wa kijiji katika kijiji hicho umevamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kitu ambacho wamesema hawakubali wako radhi kumwagike damu kama mkuu wa mkoa wa Tanga, Magalula Saidi Magalula hataingilia kati swala hilo.
Wanakijiji hao waliyasema hayo katika mkutao wao wa hadhara
uliofanyika katika kiwanja cha shule ya Msingi Segoma uliokuwa
unazungumzia swala hilo la mashamba yao pamoja na msitu wa kijijiwakidai umevamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania.
Katika barua yao wananchi hao ambayo ilitoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga ,Amina Kiwanuka ya kukabidhiwa wananchi hao mashamba yao kutoka kwa wakala wa misitu ambayo imesomwa na mwenyekiti wa kamati ya kufatilia swala hilo kijijini hapo Zuberi Fadhili.
Barua hiyo ambayo iliandikwa na kupelekewa Afisa mtendaji wa kijiji cha Segoma Ally Hamisi Madege yenye Kumb. Na.MKG/LD/F/70/47 ya tarehe 18/7/20014 ambayo ilikuwa ihahusu kukabidhiwa shamba la Sigi Segoma katika kijiji cha Segoma wilaya ya Mkinga.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya ufatiliaji shamba hilo kijijini hapo
Zuberi Fadhili akisoma barua hiyo alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga ilipoanzishwa iligawiwa shamba la Sigi Segoma lenye ukubwa wa ekari 2,829 lenye hati Na. 7675 ambapo shamba hilo hapo mwanzo lilikuwa la SHUWIMU na lilimilikishwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Muheza na baadae kugawiwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga baada ya wilaya kugawanyika.
Alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Muheza ilikuwa na kesi
mahakamani na mwekezaji CHAVDA ambayo iliisha mwaka 2011 na hivyo Halmashauri ya Muheza kushinda kesi hiyo.
Fadhili alisema kuwa baada ya hapo wataalam wa sekta ya ardhi
walifanya ukaguzi wa hali halisi ya shamba hilo kichobainika ni kwamba ekari 2,311 zimehifadhiwa msitu wa hifadhi na ekari 518 zinatumiwa na wananchi kwa matumizi mbalimbali baada ya Taarifa hiyo suala hilo liliwasiliswa katika vikao vya Halmashauri na mkutano wa baraza la madiwani kwa maamuzi.
Alisema kuwa mkutano wa baraza la madiwani ulifanyika siku mbili tarehe 16-17/7/2014 ulitoa maamuzi juu ya matumizi ya shamba hilo ambapo ekari 2,311 zilizokuwa na msitu wa hifadhi na ekari 2,311 zilikuwa na msitu wa hifadhi ambao ulikuwa unasimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania TFS zikabidhiwe katika kijiji cha Segoma ili uwe msitu wa hifadhi wa kijiji na utasimamiwa na kijiji chenyewe.
Fadhili alisema kuwa eneo la ekari 518 ambalo baadhi lilivamiwa na wananchi kwa matumizi mbalimbali linakabidhiwa katika kijiji cha Segoma ili iwe ardhi ya kijiji ambapo kijiji cha Segoma kitakuwa na mamlaka ya kugawa eneo hilo kwa wananchi wake kwa shughuli mbalimbali
za kilimo.
Aliendelea kusoma barua hiyo iliandikwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga na kutiwa sani yake ikisema ugawaji huo utafanyika kwa kufuata sheria ya ardhi ya vijiji Na.5 ya mwaka 1999 kwamba kipengele chochote cha ardhi hiyo kitakachogawiwa kiidhinishwe na mkutano mkuu wa kijiji.
Barua hiyo iliendelea kusema kuwa kijiji hicho cha Segoma kiweke
mikakati ya kulipa gharama ya kesi ambayo Halmashauri ya Muheza inaidai Halmashauri ya Mkinga ili hati ya shamba hilo iweze kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkinga na hatimae taratibu za kufutwa zifanyike ili kijiji kiweze kuandaliwa cheti cha ardhi ya kijiji na kisha utoaji wa hati miliki za kimila uweze kufanyika kwa wananchi wenye ardhi ambapo gharama za kesi hiyo watajulishwa ili waweze kulipa.
Mkurugenzi huyo aliongeza katika barua hiyo kwamba wataalam wa sekta ya Ardhi na Maliasili watafika hapo kijijini tarehe 22/7/2014 siku ya jumanne kuanzia saa 5.00 asubuhi ili kufanya kikao na serikali ya kijiji kwa ajili ya kuelekezana maelekezo hayo ambapo aliitaka serikali ya kijiji kuitisha kikao.
Hata hivyo kamati ya kufatilia swala hilo kijijini hapo waliambiwa
wapeleke fedha za gharama hizo za kesi baada ya kuambiwa na mkurugenzi kuwa ni shilingi Milioni 2.7.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa walitoka na kamati yake ambao ni
Mwanahawa Bakari,Selemani Juma Kalukoko,Julius Lukas ,Alfani Juma na Mwenyekiti wa kijiji cha Segoma Twalbu Mussa walipeleka fedha hizo ofisi ya mkurugenzi Mkinga na kumkuta kaimu wake ,Adfas Bayella lakini cha kushangaza walizikataa fedha hizo ambapo kamati hiyo ilijiuliza kunanini ndani yake.
Alisema kuwa baada ya kukataliwa kupokelewa fedha hizo waligeuza nazo ambapo waliamua kuitisha mkutano huo kuwaeleza wananchi mambo yalivyotokea huko ofisi ya mkurugenzi wa Mkinga .
Hata hivyo wananchi hao walipaza sauti zao katika mkutano huo kwa kusema Chama Cha Mapinduzi CCM hakijali wananchi wake na hivyo wanataka kura tuu na safari hii hawawapigii kura kwani wananchi wanamatatizo lakini hafiki maeneo husika.
Walisema kuwa kijiji hicho hakina Zahanati wakina mama wanazalia katika bodaboda kutokana na umbali mrefu za Zahanati lakini wamefyeka eneo ka kujenga Zahanati wamezuaia na Wakala wa Misitu Tanzani wilaya ya Mkinga wakidai eneo hilo ni la hifadhi ya msitu.
Katika mgogoro huo wananchi hao walimtaka mtendaji wa kijiji hicho Madege kutoa barua origino iliondikwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga inaonesha kukabidhiwa shamba lao wananchi ambapo mtendaji huyo alikataa kwa madai ni siri ya ofisi.
Lakini kutokana na hilo wananchi walimbeba juju mtendaji huyo wakitaka atoe barua hiyo na amkabidhi mwenyekiti wa kijiji hicho Twalbu Mussa ambapo ililazimika diwani wa kata ya Mhinduro Esam Ngatunga na Afisa mtendaji kata ya Mhinduro Challes Kaniki kuingilia kati na hivyo mtendaji huyo wa kijiji kutoa barua hiyo orgino kwa ushahidi wa maandishi.
Kwa upande wake diwani huyoalisema kuwa kikao cha baraza la madiwani wilaya ya Mkinga kikiongozwa na mwenyekiti wa madiwani Endrew Ngoda kilitoa tamko kwamba serikali ya kijiji cha Segoma wakabidhiwe shamba lao pamoja na msitu wa kijiji kutoka wakala wa mistu Tanzania.
Meneja wa Wakala wa misitu Tanzania wilayani Mkinga Frenk Chambo alisema kuwa wananchi hao wamevamia msitu wa hifadhi na kwamba kwa sasa swala hilo lipo kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Saidi Magalula hawezi kuzungumza sana.

No comments:
Post a Comment