![]() |
| Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa (CCM) kupitia mkoa mpya wa Njombe ,Hassan Mkwawa akizungumza na mwandishi wa habari David John. |
MJUMBE wa mkutano mkuu Taifa
(CCM) kupitia mkoa mpya wa Njombe ,Hassan Mkwawa amesema kuwa uchaguzi
mkuu wa mwaka huu watanzania watarajie mabadiliko makubwa ya viongozi na
hasa wabunge , kwani kutakuwa na sura nyingi za vijana.
Amesema vijana wengi wameonesha
nia na kiu kubwa ya kutaka mabadiliko hivyo kutokana na hali hiyo
kutakuwa na changamoto za kutosha kutoka kwa vijana.
Kauli ya mjumbe huyo ameitoa jana
jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini
kwake kuhusiana na mtazamo wake juu ya uchaguzi wa mwaka huu.
Mkwawa alisema kuwa vijana wana
ari kubwa na wanauwezo wa kufanya kazi ,na wapo ambao tayari wapo
Serikalini na wanachapakazi nzuri,hivyo wananchi watarajie mabadiliko
hayo.
“uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na
mabadiliko makubwa na vijana wengi watakuwa wabunge na wengi watatokana
na Chama cha Mapinduzi CCM”alisema Mkwawa.
Aliongeza kuwa hivi sasa
watanzania wanataka mtu mwenye uwezo mkubwa wa kupambanua mambo ambaye
anaweza kusimama jukwaani na kuwaeleza wananchi kwa namna atakavyo weza
kuwaletea maendeleo na si kumnyoshea mwingine kidole kwa kushindwa
kwake.
Alisema kuwa wananchi wamechoka
na siasa za kumwangalia mtu usoni na ndiyo maana katika uchaguzi wa
mwaka 2010 sura nyingi za wazee hazikupata nafasi ya kurudi katika
nafasi zao za uongozi kwakuwa walishindwa kufanya yale wananchi
waliwatuma kufanya
Akizungumzia ujio wa Chama kipya
cha ACT –wazalendo alisema kuwa chama hicho kinaonekana kukusanya watu
wengi katika mikutano yake kutokana na wengi wao kutaka kumuona Zitto
Kabwe ambapo mara zote walikuwa wakimuona kwenye vyombo vya .
Alisema kuwa katika mikutano hiyo
kuna watu ambao wanakwenda kusikiliza kinachozungumzwa kweli na wengine
wanakwenda kumuona Zitto Kabwe na kundi lingine linakwenda kutimiza
wajibu lakini, kiukweli kutokana na uwezo ambao alikuwa akionesha
bungeni ndiyo unafanya uvute watu katika mikutano hiyo.
“Zitto ni kijana na ameonesha
uwezo mkubwa wa kiongozi kiasi kwamba alikuwa akiibua hoja nyingi
bungeni,hivyo kuna vijana wengi ambao wanauwezo mkubwa wa kuongoza
watu,ambapo wengine akina January Makamba ,Said Mtanda, na wengine
wengi,alisema Mkwawa
Aidha alisema kuwa Chama cha
Mapinduzi kitashinda kwa kishindo kwani utekelezaji wa ahadi zake kwa
wananchi umekuwa wamafanikio kwa kiasi kikubwa na hata wakati wa kampeni
utakapo fika makada na viongozi mbalimbali watakuwa kwenye nafasi nzuri
ya kuelezea mafanikio hayo mbele ya wananchi.

No comments:
Post a Comment