KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 25 May 2015

SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WLF WAZINDUA MPANGO WA UZAZI




WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na ‘World Lung  Foundation(WLF)’, zimezindua kampeni ya uzazi wa mpango mkoani Kigoma.
Kampeni hiyo inakuja baada ya mkoa huo kuonekana bado uko nyuma kielimu kuhusu mpango huo ukilinganisha na mikoa mingine.
Mganga Mkuu wa Mkoa waKigomba Dk. Leonard Subi, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema mpango huo umeanza jana na kwamba utakamilika Agosti mwaka huu huku akibainisha kuwa umekuja wakati muafaka.
Alisema kampeni hiyo ya uzazi wa mpango itasidia kuokoa maisha ya akina mama kutokana na matatizo ya kiafya, kuzaa watoto walemavu na vifo ambavyo vinaweza kuchangiwa na kupasuka kwa kizazi kwa sababu ya kuzaa watoto bila ya utaratibu.
Dk. Subi, alisema kufanikiwa kwa mpango huo kutasaidia familia nyingi kuwa na afya bora ambayo itawasaidia katika shughuli za kujizalishia kipato.
“Ukosefu wa mpango wa uzazi, ikiwemo kuacha nafasi kati ya mimba moja na nyingine inachangia kuongeza vifo vya akina mama na watoto wachanga nchini,”alisema Dk. Subi.
Alisema kiwango cha uzazi Kanda ya Magharibi ikiwemo Kigoma ni watoto saba ikilinganishwa na wastani wa watoto watano kwa Tanzania na wastani wa watoto 2.5 duniani.
Naye Mkurugenzi waTaifa wa WLF, Dk. Nguke Mwakatundu, alisema kampeni hiyo inajulikana kwa jina la Thamini Uhai, iliyoanza mwaka 2014 ilitilia mkazo muhimu wa kujifungua katika kituo cha afya.
Alisema data iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiria kuwa ingawa mwaka 2010 idadi ya vifo vya akina mama nchini ilikuwa asilimia 3 ya vifo vyote vya uzazi duniani.
 Hata hivyo, Dk. Mwakatundu, alisema Tanzania kupunguza kiwango cha vifo vya uzazi kwa asilimia 55 kati ya mama na watoto wachanga nchini kwa kutekeleza mradi unaotumia teknolojia na vifaa vya kisasa.

No comments:

Post a Comment