KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday, 5 June 2015

SEVERINE: MRAMBA HAJAHUDHURIA MKUTANO WOWOTE WA KISIASA



Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Maramba

MSEMAJI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Adrian Serine amesma Mkurugenzi  Mtendaji wa shirika hilo, Felchesmi Mramba, hajahudhuria wa wala kuandaa mkutano wowote wakisiasa.
Severine, alisema hivyo wakati alipokuwa akikanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii juzi kwamba Mkurugenzi huyo, alikuwa miongoni mwa wajumbe 17 wanaodaiwa kuandaa moja wapo  ya mikutano ya kisiasa katika hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, msemaji huyo, alisema ingawa taarifa hiyo haikufafanua jina la mkurugenzi mtendaji huyo wa Tanesco, kwa kutoweka wazi, zinaamanisha ni Mramba hivyo shirika linawataka wananchi kuzipuuza kwani sio sahihi na zinalenga kumharibia mkurugenzi huyo.
“Katika taarifa hii  haijulikani  kama mkurugenzi mtendaji  ni nani anayetajwa kwani kiongozi mkuu wa tanesco hajatanjwa jina basi taarifa hizi zinamaanisha mkurugenzi mtendaji ambaye ni basi si sahihi,”alisema Severine.
Alisema,  hivyo kwa vile Mei 29 mwaka huu, inayotajwa katika taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji alikuwa na mkutano wa wafanyakazi  wote wa makao makuu ya shirika hilo na wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuanzia saa 7:00  mchana hadi saa 12:00 jioni , uliofanyika Ubungo na kwamba Mkurugenzi huyo asingeweza wakati huo huo kuwapo mjini Arusha.
Severine alisema kuwa Mkurugenzi huyo Mei 30 alisafiri kikazi nje ya nchi ambako hadi sasa hajarejea nchini.
Aidha, mkurugenzi wa  tanesco ni mtumishi wa umma anaongozwa na kanuni za utumishi wa  umma  zinazomtaka kutojihusisha kwa namna yoyote  na masuala ya kisiasa, kanuni ambazo mkurugenzihuyo anazifahamu vizuri.
Severine alisema kutokana na kanuni hizo, anaamini kuwa mkurugenzi huyo asingeweza kufanya hivyo, kwani kufanya hivyo ni sawa na kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
“Ikumbukwe kuwa Tanesco ni shirika la kiufundi na lipo kwa manufaa ya Watanzania  wote,’alisema Severine.
Aliongeza kwa kusema kuwa mkakati wa shirika  kwa sasa ni kushughulikia changamoto za umeme nchini na kuhakikisha nchi ina umeme wa uhakika, mkakati ambao ambao mkurugenzi mtendaji ndiye msimamizi wake.

No comments:

Post a Comment