KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday, 10 July 2015

JMII YATAKIWA KUKUMBUKA WATOTO YATIMA

Baadhi ya Wanalyalamo wakijumuika na watoto wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund.
WITO umetolewa kwa Watanzania kujitolea kwa hali na mali kusaidia watu wenye uhitaji maalumu ikiwemo watoto yatima wanaolelewa katika vituo vituo malimbali.
Wito huo umetolewa jijini juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Yatima GroupTrust Fund kilichoko Chanika, Dar es Salaam, Winfrida Lubanza, wakati alipozungumza na wanafamilia wa Lyalamo.
Alisema jamii inapaswa kuwakumbuka watoto walioko katika vituo hivyo kwa vile wanastahili kupata mahitaji ya kibinadamu kama ilivyo kwa watoto walioko majumbani.
“Watoto yatima ni watoto kama wengine nao wana uhitaji sawa hivyo jamii isiwasahau na kwani nao wanapata faraja na kupata matumaini zaidi wanapokumbukwa,”alisema.
Aliongeza kwa kusema kuwa kituo chake kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo chakula, dawa, sabuni na ada kwa wanafunzi sambamba na mtaji wa kuwezesha kuanzisha biashara ambayo itaweza kuwapatia fedha za kujikimu.
“Tuna changamoto nyingi mfano kuna mwanafunzi ambaye yuko kidato cha nne amerudishwa kituoni kwa sababu hatujakamilisha ada,”alisema.
Naye kiongozi wa Lyalamo Family, Aziza Kibwana, alisema wamefarijika kufika kituoni hapo na kujionea changamoto hizo, watajitahidi kuchangia walichojaliwa.
Pia alisisitiza wadau wengine kujitokeza katika kusaidia vituo vinavyolea watoto hao, baadhi yao watakuwa wataalamu wa kesho katika taifa hili.
“Sisis tumesoma shule ya msingi boarding tukiwa wadogo na tulikuwa na watoto kutoka katika vituo kama hivi hivyo tunaguswa sana na hali zao ndio maana tuko hapa.
Humu kuna marais, kuna wabunge, wanasoka, wasanii, wafanyabiashara, madaktari, wahasibu nakadharika sasa ni muhimu kuwakumbuka na watoto walioko huku ili kuwajengea misingi mizuri yay a kutimiza ndoto zao,”alisema.
Katika ziara yao hiyo walikabidhi kituo hicho vyakula, mafuta, dawa, madatari, sabuni na vitu vingine ambapo watoto walioko kituoni hapo walifurahi na kushukuru.
Kituo hicho kilianzishwa mwaka 2001, hadi sasa kinalea watoto kati ya150 hadi 300 wenye umri wa kuanzia mwaka 0 hadi miaka 18.

No comments:

Post a Comment