KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 22 July 2015

MKUTANO WA MAADILI YA UCHAGUZI WAVUNJIKA

Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati).
MKUTANO wa kusaini maadili ya uchaguzi kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Vyama vya Siasa, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Otoba 25 mwaka huu umevunjika baada ya vyama kupinga kusaini kutokana na kunyofolewa baadhi ya kurasa katika kitabu cha maadili hayo.
Kwa mujibu wa maadili hayo, kila Chama Cha Siasa na kila mgombea atawajibika kusaini maadili hayo, chama ambacho hakitasaini kitazuiliwa kushiriki katika kampeni za uchaguzi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Kijamii (CCK), Renatus Muhabhi, alisema vyama hivyo vimeitaka NEC kuacha mzaha na suala la uchaguzi.
 Alisema, chanzo cha kuvunjika mkutano huo kumetokana na hoja ya wajumbe wa kuwa hawangeweza kusaini hayo bila ya kuyaona yale waliyokubaliyana katika mikutano miwili iliyofanyika awali.
Muhabhi, alisema baada ya hoja hiyo wajumbe wote wakaunga mkono hoja hiyo, ikabidi Mkurugenzi wa NEC, agize yakaletwe lakini cha kushangaza yalipoletwa ikabainika kulikuwa na upungufu wa kurasa 10 katika ya 24.
 “Ilikuwa sio rahisi kusainishwa fomu bila ya kuyaona mezani na kuyapitia makubaliano waliyoyaainisha katika vikao viwili vilivyopita ambapo yapo waliyoyafanyia marekebisho,”alisema Muhabhi.
Muhabhi, alisema pamoja na sintofahmu hiyo, Mkurugenzi wa NEC, alishindwa kuwaeleza wajumbe sababu haswa zilizofanya kuosekana kwa kurasa hizo na ilikuwa ni kwa maslahi ya nani.
Alisema, baada ya mvutano huo wajumbe wote kwa pamoja waliungana na kuamua kuvunja kikao hicho huku wakiitaka Tume kuwa inahakikisha kuwa inayafikisha makubaliano ya awali kabla ya kutiwa saini Jumatatu ijayo. 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philp Mangula, alifoka na kusema kwamba serikali imekuwa ikilaumiwa kutokana na uzembe wa mtu mmoja.
Mangula, alisema inaonekana Mkurugenzi alikuwa haijajipanga kwa hiyo amekurupuka hivyo basi  wajumbe wanapaswa waeleze kilichotokea sababu iliyosababisha hali hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura, alisema ilibidi wavunje mkutano huo baada ya Katibu Mkuu wa CCK, Muhabhi kuibua hoja ya kutaka waletewe fomu za vikao viwili vilivyopita.
“Kwa kweli kitendo hicho kilimsikitisha Katibu Mkuu wa CCM, ambaye aliwalaumu kwa kuwaambia ndio Tume kwamba wanasababisha serikali ilaumiwe kama, walikuwa hawajajiaandaa ilikuwaje watuite,”alisema Sungura.
Sungura, alisema baada ya Mkurugenzi hatua hiyo imemkasirisha Mangula, alionekana kuwa karibu na katibu mkuu huyo, mithiri ya mtu aliyekuwa akitaka kuomuomba radhi.
“Tulika kama dakika 25 muda wa kuwasubiri kwa ujumla mazungumzo yote yamechukua muda huo, inasikitisha kwani kulikuwa kumekosekana karatasi kama 13,”alisema Sungura.
Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba, alipotakiwa kuzungumzia kadhia hiyo alijibu kwa sauti ya upole na kwa kifupi kwamba mkutano huo haukuvunjika bali ulikuwa umeahirishwa na kitaendelea Jumatatu ijayo.
Hata alipotakiwa kutoa sababu za kuahirishwa mkutano huo ndani ya dakika 25 tangu kuanza: Haujavunjika ni nani aliyekwambia kama ni sababu waulizeni hao waliowaeleza, lakini kikao tumekiahirisha.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid, aliwaomba radhi wajumbe baada ya kuambiwa na Mangula kwamba walikuwa hawajajipanga na ndio maana mkurugenzi anafanya kazi za hovyo hovyo.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damiani Lubuva hakuwepo katika mkutano huo ikidaiwa kuwa yuko nje ya nchi.


No comments:

Post a Comment