KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday, 14 August 2015

KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA UPANGA MAGHARIBI ANUSURIKA KIPIGO

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Kinana
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Upanga Magharibi, Abdul Malilima, amenusurika kipigo baada ya wanachama wenzake kudai kuwa amevuruga kura za maoni za diwani  na mbunge kwa kwa ajili ya kumsaidia Adnan Kondo aweze kushinda.
Wanachama hao walifikia hatua hiyo baada ya kubaini njama za katibu huyo ambaye alihamishiwa katika Kata hiyo siku mbili kabla ychaguzi huku wakidai alipelekwa kwa mkakati maalumu wa kumsaidia mshindi huyo ambaye ni mtoto wa Waziri wa Jinsia na Watoto Sofia Simba.
Akizungumza na wandishi wa habari, nje ya Ofisi za Kata hiyo jijini Dar es Salaam leo, Balozi wa Nyumba ‘10’ Ashraf Khan, alisema wanaopaswa kulaumiwa katika kuvurugika uchaguzi huo ni viongozi wa Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa.
Alisema, wamefikia hatua hiyo kutokana na kitendo cha katibu huyo cha kuwanyima haki ya kupiga kura wanachama wa tawi la Upanga Maghari na Muhimbili huku akitoa nafasi hiyo kwa watu kutoka matawi mengine jijini.
“Kata yetu ina matawi manne lakini cha kushangaza ni matawi mawili ambayo ni Tambaza na Minazini ndio yafanya uchaguzi ambao ulitawaliwa na ukiukwaji wa sheria kwani waliopiga kura ya kumchagua Adnani sio wakazi wa matawi hayo,”alisema Khan.
Alisema, kuwa kura hiyo ya maoni inayodaiwa kufanyika katika matawi hayo hawaitambui kwa vile wapiga kura wengi walisafirishwa kutoka Mbagala, Manzese, Mabwepande na wagonjwa (mateja), wanaotumia dawa za Methodine katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili.
“Tunawaomba viongozi wa ngazi ya juu wa chama kutambua kuwa kura za mbunge Azan Zungu zilizopelekwa Dodoma hazikutokana na wanachama wa Upanga Magharibi kwani siku ya kupiga kura hata kitabu cha orodha ya majina ya wapiga kura kilifichwa nyumbani kwa katibu huyo,”alisema Khan.
Vurugu hizo zilizidi zaidi pale Katibu huyo alipogoma kutoka nje ya ofisi ili azungumze na wandishi wa habari, hali iliyowafanya wanachama hao kutoa kwa nguvu huku wakilazimisha azungumze.
Hata hivyo,  Malilima aliamuwa kuzungumza kwa unyonge aliamua kuyaacha matawi hayo mawili katika kura hiyo ya maoni kutokana na maelekezo aliyopewa bila kufafanua, yalitoka wapi.
“Mimi nimeamua kuzungumza lakini kwa vile mnafanya vurugu nafikiri sitakuwa tayari kuzungumza na wahuni,”alisema Katibu huyo.
Baada ya kugoma wanachama hao walimnyang’anya funguo ya Ofisi na kumfukuza huku wakimwita mwizi wa kura, wakimtaka kutorejea tena katika ofisi hiyo kwani hata atakaporudi hawako tayari kumpa ushirikiano.
Naye Beatrice Makan, ambaye ni mmoja wa viongozi katika Kata hiyo, alisema kuwa uchaguzi huo matokeo yake yalipangwa na viongozi wa CCM Mkoa huo kwa lengo la kumsaidia mtoto wa waziri huyo.

Alisem baada ya uchaguzi huo kuvurugika Agosti Mosi, Ofisi ya CCM wilaya iliagiza urudiwe lakini cha kushangaza haukurudiwa na baadala yake matokeo yalipelekwa Dodoma yakionesha kuwa matawi yote yalipiga kura hiyo wakati sio kweli.

No comments:

Post a Comment