SHEIKH Mkuu wa Baraza Kuu la Waisilam (Bakwata), mkoani Dar
es Salaam, Alhad Mussa Salum huenda akaingia matatani kutokana na kauli yake kuwa
kiongozi wa Uamsho, Amir Farid Had Ahmad, ameunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi Zanzibar.
Juzi wakati akizumgumza na wandishi wa habari jijini Dar es
Salaam juu ya mkwamo wa kisiasa unaondelea Zanzibar, Alhad Salum, alisema kwa
sasa njia pekee ya kumaliza mgogoro huo ni kurudiwa uchaguzi, kwani hata Amir
wa Uamsho Sheikh Farid Hadi Ahmed pia anaunga mkono.
Akizungumza jijini leo, Wakili, Juma Nassor, alisema hayo wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi
kuhusu ukweli wa mteja wake, Sheikh Farid kama kweli ameandika barua hiyo ya
kuunga mkono, iliyooneshwa mbele ya wandishi wa habari kama na Sheikh Alhad
Salum.
Nassor, alisema Sheikh Alhad Salum, anaweza kuingia matatani
endapo kama Sheikh Farid, atalalamika na kulifikisha kwenye vyombo vya sheria madai hayo kutokana
na taarifa hizo kutangaziwa Umma kwamba aliandika barua iliyokuwa na mambo
matatu moja likiwa hilo la kuunga mkono kurudiwa uchaguzi.
“Kuhusu nini kifanyike kutokana na kitendo cha Alhad Salum,
hiyo itategemena na Sheikh Farid mwenyewe kama atamua kufikisha malalamiko
kwenye vyombo vya sheria lakini pia anaweza kuamua kusamehe, uamuzi ni wake,”alisema
Nassoro
Hata hivyo, wakili
huyo, alisema kuwa viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), tayari wamekwishasema kupitia majukwaa ya siasa kwamba
Zanzibar ni nchi iliyotawaliwa baada ya kufanyika mapinduzi hivyo haiwezi
kutolewa kwa njia ya makaratasi yaani uchaguzi.
Akizungumza
na wandishi wa habari jijini juzi Siku ya Jumanne, , Alhad
Salum, alisema kusudi kubwa la kukutana nao ilikuwa ni kutoa salam za pongezi
kwa serikali ya awamu ya tano kutokana na kitendo chake kuimarisha nidhamu kwa
watumishi wa Umma na wale wa serikali.
Alisema,
Bakwata, imefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa hakuna njia mbadala ya
kumaliza gogoro huo, zaidi ya kurudiwa uchaguzi.
“Kwa
sasa hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza
mgogoro huo, kwani hakuna njia mbadala hata Amir wa Uamsho Sheikh Farid Hadi
Ahmed pia anaunga mkono suala la hilo la kufanya uchaguzi wa marudio kwa mujibu
wa barua yake aliyonitumia mimi toka Gerezani.
Hivyo
basi naomba kuchukua fulsa hii kukiomba Chama cha Wananchi (CUF), amabacho tayari kimekwishatangaza kususia
uchaguzi huo wa marudio na Vyama vingine vyote vya siasa vilivyoko Zanzibar
viache kususia uchaguzi huo,”alisema Alhad.
Alisema
baadala ya kususia uchaguzi huo ni vema vikajipanga kwa ajili ya kushiriki na
huku akiomba ZEC kuhakikisha kuwa inasimamia uchaguzi huo kwa kuzingatia haki,
uadilifu na umakini mkubwa kwa masilahi ya Taifa.
“Tunawaomba
Wazanzibar wadumishe amani na utulivu walionao na kulinda umoja na mshikamano
wao kwa kuwa wao ni ndugu,”alisema Alhad.
Kazungumzia
mafanikio ya serikali ya awamu ya tano, Alhad alisema anaipongeza kutokana na
dhamira yake ya kubana na kupunguza matumizi ya serikali yasiyokuwa ya lazima
na baadala yake kuelekeza fedha kwenye huduma za kijamii.
Alisema
kutokana utaratibu huo, tayari Watanzania wameanza kunufaika na huduma kama
vile suala la elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne huku
akibainisha kuwa ni jambo jema linalopaswa kupongezwa.
“Kwa
kuwa ada za shule na gharama za kuandikisha watoto wanaoanza darasa la kwanza
ulikuwa mzigo mkubwa kwa wananchi walio wemgi, pamoja na kuboresha huduma za
Afya kwenye Hospitali za serikali,”alisema Alhad.
Alisema
pamoja na pongezi hizo lakini pia Bakwata inaiomba serikali izidi kupambana na
changamoto mbalimbali hasa zote zilizoko ndani ya jiji hilo hususan suala zima
la foleni ambalo linachangia kuzorotesha uchumi wa Taifa.
Alhad,
alisema pia kuna haja kwa serikali kumaliza mvutano uliyojitokeza kati ya wadau
wa usafirishaji na Sumatra juu ya kiwango cha nauli za Mradi wa Mabasi yaendayo
Haraka (DARTS).
Alhad,
alisema anaamini kuanza kwa mradi huo kuna weza kuwa mkombozi katika kupunguza
changamoto hiyo ya foleni katika jiji hilo.
No comments:
Post a Comment