WAKAZI wa Kijiji cha Mubunda wilayani Muleba mkoani Kagera wameilalamikia serikali kutokana na kushindwa kukamilisha kwa wakati mradi wa maji ili waweze kuondokana na adha wanayoipata ya kufuata huduma hiyo mbali.
Wakazi hao waliyasema hayo baada kuona mradi huo wa maji
uliyoanzishwa Januari mwaka 2014, ulitakiwa kukamilika Januari mwaka jana
kushindwa kukamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa.
Ujenzi wa mradi huo ambao ulitarajiwa kumaliza kero ya
wananchi kuhangaikia huduma hiyo huku wakitumia maji ambayo ni hatari kwa afaya
zao, umeigharimu serikali sh.Milioni 900.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam juzi, kwa niaba ya wakazi wenzake aliyongozana nao, James Muga alisema
pamoja kudaiwa kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 99, hata hivyo, wakazi
hao hawaamini kama ujenzi huo unalingana na thamani ya fedha iliyotumika katika
ujenzi wake.
Alisema, hatua ya kuuzungumzia mradi huo kupitia vyombo vya
habari kumesababishwa na wasimamizi wa utekelezaji wa mradi huo kushindwa kutoa
sababu halisi zinazo kwamisha kukamilika mradi huo ambao ujenzi wake ulipangwa
kuwa wa mwaka mmoja na ambao umeishapita tangu januari mwaka jana.
“Hatuelewi sababu inayokwamisha mradi huu, wanatuambia
mradi umekamilika kwa asilimia 99 lakini tangu tulipoambiwa mwaka jana hadi
sasa mwaka mmoja umepita tunashangaa haujaanza kutoa huduma iliyokusudiwa.
“Wakati wakiendelea kutoa sababu zinazojichanganya kwamba
mara mradi umekamilika asilimia 99 kilichobaki ni kuzinduliwa lakini pia
utasikia hivi sasa wanasubiri hela za kununulia mashinde za kusukuma maji sasa
hatuelewi tushike lipi lakini yoye kwa yote wananchi ndiyo tunaoathirika kwa
kukosa huduma hiyo muhimu,”alisema Muga.
Akitolea ufafanuzi malalamiko hayo Diwani wa Kata
Mubunda, Kalinjuma Kamili, alisema mradi
huo hadi sasa umefikia asilimia 85 na wala siyo 99, kilichojitokeza ilikuwa ni
kukosekana kwa mashine ya kusuma maji.
“Unajua awali mradi huo ulipangwa itumike mashine ya
kusukuma maji lakini baadaye ulipokuja umeme wa REA ndiyo wakaona siyo vizuri
kutumia mashine kwa sababu umeme ni bora zaidi,”alisema Kalinjuma Kamili
Kalinjuma Kamili alisema baada ya makubaliano kati ya
Mkurugenzi na Mkandarasi ya kubadili mfumo wa awali tayari kwa siku ya jana
mkandarasi imekwishaanza kufunga vifaa hivyo vinavyotumia umeme kwa hiyo
wakikamilisha huduma hiyo itaanza kupatikana kuanzia leo.
“Kweli kulikuwa na changamoto iliyosababisha kuchelewa
mradi huo ili kuwa ni kukosekana kwa fedha na siyo mradi huu pekee bali ilikuwa
yote iliyokuwa ikifadhiliwa na Benki ya Dunia ilisimama,”alisema.
Kuhusu, kujengwa chini ya kiwango, Kalinjuma Kamili,
alisema hawezi kukbaliana na kauli ya wakazi hao, kwa sababu hatua zote za
ujenzi zilizokuwa zikifanyika alizishuhudia lakini pia Mkurugenzi alikuwa
anapitia kila hatu wakati ujenzi wa mradi huo ilipokuwa ukiendelea.
Alisema, anaweza kukubali hilo baada ya kufungwa mashine
hizo, nakushindwa kutoa maji hapo ndiyo anaweza kukubali lakini kwa sasa
hakubalini na hilo kwa vile tangu hatua za ujenzi wa matenki na kulazwa kwa
mabomba alishuhudia kwa kuwa bega kwa bega na makandarasi.
WISHO
No comments:
Post a Comment