WAKAZI wa jiji la
Dar es Salaam wameshangazwa na ukimya wa uongozi wa Mkoa huo, wa kuvifumbia
macho vitendo vya kinyama vinavyofanywa na polisi wakati wa wanapofanyakazi ya
kukamata pikipiki (Bodaboda), wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) na
Mamalishe.
Hatua ya kukamata
bodaboda inatokana na agizo la mkuu wa mkoa huo ambalo linawataka madereva wa
bodaboda kutoingia akatikati ya jiji ambalo amelitoa zidi ya miezi mitano
iliyopita.
Wakizungumza na
BLOGG hii jijini leo, walisema vitendo wanavyofanyiwa madereva wa bodaboda,
inasikitisha kwani vinakiuka haki za binadamu.
Kwa niaba ya
wenzake, Jafari Yahya, alisema kutokana ukimya huo, wakazi haowanamuomba waziri
mkuu mizengo pinda kuchukua hataua za haraka ili kukomesha vitendo hivyo
ambavyo vimekithili.
Alivitaja vitendo
hivyo kuwa ni kuporwa mali za wafanyabiashara hao pia kuumizwa madereva wa
bodaboda pamoja na abiria wanaopakia kutokana na kukimbizwa hovyo bila kujali
sheria za usalama barabarani wakati polisi wanapotaka kuwakamata.
“Ukiangalia askari
hawa, moja kwamoja utaona wanalitumia agizo la mkuu wa mkoa kama kigezo
cha kujihalalishia kufanya unyang’anyi wa mali za walala hoi hawa ambao
wamepigika kimaisha,”alisema Yahya.
Yahya, alisema
mamalishe, bodaboda na wamachinga wamekuwa hawana raha kutikana na kuporwa mali
zao mchana kweupe kigezo ikiwa ni agizo la mkuu wa mkoa, hali ambayo inawafanya
wananchi wanaoshuhudia matukio hayao kuungana na wafanyabiashara hao kuichukia
serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, alidai kuwa polisi
hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo bila ya kuwa na muda maalum mfano utawaona
majira ya saa 12:00 jioni wakikamata mali za watu kama vile nguo, mabegi na
simu na kichoshangaza wanaondoka nazo mbio katika gari bila ya mwenye mali.
Alisema, akama
serikali haitakuwa makini na chuki na hasira zinazozidi kuongezeka dhidi ya
vitendo wanavyofanyiwa huku serikali ikiwa kimya kuna hatari uvumilivu wa
wananchi siku moaja ukaja kutoweka na kitakachotokea wakati huo hakitajulikana.
“Kinachofanywa na
polisi ni wizi, unyang’anyi ambao uko sawa na ule wakutumia nguvu kwani
wanakuja na silaha na gari wanachukuwa mali zaraia ambao hawana silaha na
kutokomea nazo kusikojulikana.
“Wafanyabiashara
hawa hawajamdhulu mtu mwingine, ni ajabu kama mtu anajitafutia kipato kwa uhalali
halafu vyombo vya doala vinawapinga kwa kweli sheria hiyo tunaishangaa
sana,”alisema Yahya.
No comments:
Post a Comment