KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 26 February 2015

KIGOGO TBA APATA CHEO KWA NJIA ZA UDANGANYIF

KIGOGO mmoja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), inadaiwa kuwa amengia kwenye kashfa ya kutumia njia za udanganyifu katika kujipatia wadhifa alionao sasa.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya ofisi hiyo, kililiambia BLOG hii, kuwa udanganyifu huo umetokana na mchakato mzima uliyomfanya kigogo huyo apate cheti baada ya mtihani uliyofanyika mwaka 2012 unatia shaka.
Kilisema kuwa kigogo huyo, alijipatia cheo hicho bila ya kufuata utaratibu unaotakiwa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha cheti toka Bodi ya Usajili wa Wasanifu na Wakadiriaji wa Majengo katika tume ya ajira, wakati vyeti vya watahiniwa waliofaulu vikiwahavijatoka.
“Mitihani ilifanyika Juni 2012 na matokeo yametangazwa Julai 31, 2012 na vyeti vikiwa havijaandaliwa lakini yeye aliwakilisha cheti Juni kabla  ya vyeti kutolewa kitendo kilichomfanya ajipatie cheo kwa udanganyifu.
“Pia kutokana na elimu yake hakuruhusiwa kufanya mtihani wa mwisho kabla ya ‘Intermediate’  lakini kwa mshangaao Bodi ikamruhusu hivyo kukiuka sheria na taratibu za usajili.
Chanzo hicho kilisema Msajili wa zamani wa Bodi Architect, Meresi alimzuia asifanye mtihani wa ‘Final’ bali alitakiwa aanzie na ‘Intermediate’ lakini alifanya mtihani huo katika mazingira yenye utatanishi, ili tu apandishwe cheo isivyo halali.
Uwamuzi wa Architect, Meresi kuzuia kigogo huyo kulijenga chuki kati yake na Waziri wa Ujenzi kwa vile waziri huyo anadaiwa kuwa alikuwa karibu na kigogo huyo.
“Chuki hii ililimfanya waziri huyo wa ujenzi kumtukana Architect, Meresi alipokwenda kwenye semina ya Bodi Morogoro,”Kilisema chanzo hicho.
Aidha kigogo huyo aliamua kununua samani zenye thamani ya sh milioni 40, ambazo alidai kuwa zilikuwa za Rest-House ya Ujenzi Dodoma wakati haikuwa kweli.
Chanzo hicho kilisema, kumbe samani hizo ili kuwa ni kwa ajili ya kulipa fadhala kwa waziri wa ujenzi ambaye ametumia madaraka yake vibaya ya kumpatia kigogo huyo cheo hicho bila ya kufuata taratibu.
“Samani hizo pamoja na jakuzi lenye Luninga, kwa kujua kitendo hicho siyo halali samani hizo zilisafiriswa usiku na gari T 246 ANU mali ya Wakala Mkoa wa Dar es Salaam likiendeshwa na dereva (Jina tunalo na namba yake ya Simu).
“Samani hizo zilipokewa na mmoja wa vigogo wa TBA Dodoma (jina na namba yake yasimu tunavyo), ambaye baadaye alizipeleka numbani kwa Wzairi,”kilisema Chanzo hicho.

Aidha, juhudi za kumpata kigogo huyo zinaendelea ili aweze kutoa ufafanuzi kuhusu madai hayo na mengine ambayo yanahusiana na utoaji wa nyumba kwa kutumia kigezo cha ukabila.

No comments:

Post a Comment