NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA
la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), limeandaa madawati ambayo
yatatumika kupokea malalamiko na kutoa elimu katika maadhimisho ya Wiki ya Maji
inayoanza leo hadi Machi 22 Mwaka.
Taarifa
iliyosambazwa kwa vyombo vya habari ikisainiwa na Ofisa Uhusiano wa Dawasco, Everlasting
Lyaro, alisema madawati hayo yakuwepo
katika Ofisi zake za Makao Makuu zilizoko barabara ya Sokoine Drive, Kinondoni
na Boko.
Lyaro,
alisema licha ya kutoa elimu pia itapokea maoni ya wateja lengo likiwa
kuwaelimisha wananchi wa mkoa huo kuhusu sera ya maji.
“Kuna
program zinazoenelea za ujenzi wa miradi ya maji, mipango ya baadaye na umuhimu
wa ulinzi wa miundombinu ya maji na matumizi sahihi ya dira za maji,”alisema
Lyaro.
Alisema
madwati hayo yakuwa wazi katika pindi hicho cha wiki nzima kuanzia Machi 16
hadi Machi 22 mwaka huu, kuanzia saa 2 Asubuhi hadi saa 12 jioni kila siku.

No comments:
Post a Comment