KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 15 March 2015

BALOZI MWAPACHU AWA MWENYEKITI AIRTEL TANZANIA

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Bharti Airtel imemteua Balozi Juma Mwapachu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel Tanzania.

Balozi Mwapachu ni Katibu Mkuu aliyepita wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, nafasi aliyoishika kati ya Aprili 2006 na Aprili 2011.  Kabla ya uteuzi huu, Mwapachu alikuwa Balozi Mwakilishi Ufaransa na UNESCO.

Akizungumzia uteuzi huo mjini Nairobi, Kenya juzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Afrika, Christian de Faria, alisema ni faraja kwao Balozi Mwapachu kuiongoza Bodi yao ya Wakurugenzi 

Tanzania, kwani ana uzoefu mkubwa utakaoongeza thamani kubwa kwa bodi yao.
Kwa upande wake, Balozi Mwapachu alisema mepokea kwa heshima kubwa fursa hiyo na atashirikiana na wajumbe wenzake wa bodi hiyo kujenga kampuni thabiti yenye misingi imara, ili kuendelea  kutoa huduma bora ya mawasiliano nchini Tanzania.


 “Ukuaji wa teknolojia ya hali ya juu na ubunifu katika masoko ikisaidiwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa sekta hii ni dhahiri kutakuwa na uwezekano kwa sekta hii kuendelea kutoa mchango mkubwa  kwa taifa,” alisema.

No comments:

Post a Comment