| Hizi ni baadhi ya chupa za mikojo zilizotelekezwa juzi na watu wasiojulikana katika makutano ya Mtaa wa Azikiwe na Samora, jijini Dar es Salaam juzi |
NA MWANDISHI WETU
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watu wasiyojulikana walitupa fuko kubwa ambalo lilikuwa limejaa chupa zilizojaa mikojo.
Tukio hilo limetokea baada ya siku moja taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), kutoa matokeo ya utafiti uliofanywa mwaka 2014 kwamba vyombo vya plastiki na matairi ya magari, zilivyojaa maji yana changia kwa kiasi kikubwa kuzalisha mbu waitwao ‘Aedes aegypti’wanaoambukiza ugonjwa wa Dengue.
Fuko hilo kubwa ambalo lilijaa chupa hizo za mikojo huku nyingine zikiwa zimesambaa lilikuwa limetupwa katika makutano ya Mtaa wa Azikiwe na Samora, kwenye mzuunguuko wa Sanamu ya Bismini jinni Dar es Salaam juzi.
Mwandishi wa habari hizi ilishudia kundi kubwa la wananchi wakishuhudia uchafu huo, huku kila mmoja akisema lake.
Joseph Ubango mkazi wa Kigamboni alisema kuwa kutupwa kwa mafuko ya mikojo katika eneo hilo si mara ya kwanza, lakini kinachomshangaaza ni kutochukuliwa hatua watu wanaofanya hivyo.
“Unajua wale wanaosema kuwa Tanzania inaongoza kwa uchafu katika nchi za Afrika Mashariki au hata Afrika nzima mimi naona hawajakosea,”alisema.
Ubango, alisema eneo lilikotupwa fuko hilo palisambaa harufu mbaya iliyowafanya wapita njia kuziba pua walipofika hapo.
Pamfil Shayo, Mkazi wa Mwembe Yanga, alisema eneo hilo limekuwa likifanywa kama dampo.
Alisema, kuwa aliwahi kushuhudia fuko kama hilo lilikiwa limejazwa kinyesi na kutelekezwa katika eneo hilo.
Shayo, alisema anashangazwa na Mamlaka ya Jiji kushindwa kuwaelekeza askari wake kufuatilia vitendo hivyo na baadala yake wamekuwa wakisumbuana na mamalishe wasiochafua mazingira.
“Jiji hili halina vibweta vya kutupa taka kama watu watakuwa na kumbukubu kuna kamuni moja ya kufanya usafi iliwahi kutangaza kwamba itahakikisha kuwa kila baada ya mita 200 itaweka vibweta hivyo lakini hakuna hata kimoja,”alisema Shayo.
Shayo alisema hali yakukosekana vibweta hivyo, inawafanya wakazi wa jiji hili kutembea na chupa za maji mikono kutokana na sehemu ya kuzitupia ama wengine huamua kuzitupa hovyo hadi zije kuokotwa na vijana wanaofanya kazi ya uuza chupa tupu za plastiki.
No comments:
Post a Comment