KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday, 6 March 2015

KIKWETE AZINDUA STUDIO YA KISASA

RAIS Jakaya Kikwete, amevitaka vyombo vya habari, kuwa vinahakikisha vinatangaza matangazo yenye kuzingatia sheria na maadili ya Watanzania.

Kikwete, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Studio ya kampuni ya Azam Media Group Limited, ambayo ni ya kisasa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Hadi kukamilika kwa ujenzi wa studio hiyo umegahrimu sh bilioni 53.

Alisema hivyo kwa vile televisheni hiyo hivi sasa itaonekana kimataifa, hivyo isije ikawafanya wakashawishika kuwasahau Watanzania na kuanza kurusha vipindi ambavyo vitakwenda kinyume na sheria za nchi.

Aidh, alisema serikali haitaona haya, lazima itasema pindi itakapoona baadhi ya vyombo hivyo habari vinatoa bari za hovyo, ambazo msingiwake ni kuipotosha jamii na atakayekwenda kinyume lazima atabawa na sheria.

 Kikwete, alisema bado serikali inatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika jamii, akiahidi kuwa itaendelea kuweka mzingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya habari.
“Hatuna wasiwasi na vyombo vya habari tunataka viendelee kuwepo ila view vinafuata maadili.

“Uhuru wa vyombo vya habari sio kutangaza habari yoyote huo utakuwa sio uhuru wa habari bali hiyo ni vumai ya habari,”alisema.

Rais Kikwete, alisema hawatakubali kuona baadhi ya vyombo vya habari vinatumia uhuru huo vibya kwa kutangaza habari za uchezi, chuki na vuruma katika jamii.
‘Lakini ukisema serikali ya CCM imeshindwa hilo halina madhara na siwa,”alisema Rais Kikwet.

Akizungumzia Azam Media, Rais Kikwete, aliutaka uongozi wa kampuni hiyo kujikita zaidi katika kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake ili waweze kwenda mabadiliko ya kiteknolojia.
Alisema kwa kufanya hivyo kutawasaidia kuwa na wafanyakazi wenyeueledi na bora zaidi kiutendaji.

“Mafunzo ni muhimu kwenye kazi kinyume chake mtakuata utendji wao wote unashuka na watakuwa wakitoa habari mbaya,”alisema.

Pia Rais Kikwete, alisistiza suala mishahara kwa wafanya kazi wao kama hawakuliangalia hilo watambue kuwa watalipwa mitaani kitendo kitakachowafanya watowe habari za hao waliowapa.    

Rais Kikwete, alipongeza uongozi wa Azam kwa kujenga studio ambayo alisema hajapata kuiona katika ukanda huu.
Mtendaji Muu wa Azam Group, Saidi Bakhresa, alisema haikuwa rashisi kukamilisha mradi huo kwani ilikuwa ni shughuli pevu.

Alisema kikubwa anaishukuru serikali kwa kutoa fursa sawa katika uwekezaji, ambapo pia aliwashukuru Watanzania kwa kuwaunga mkono katika matumizi ya bidhaa zao.

 Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Tido Mhando, alisema Studio  hiyo ni yakisas, ambayo italeta mapinduzi katika utangazaji wa televisheni nchini.  
 “Studio zetu ni za kisasa zaidi ndani ya Afrika Mashariki na Kati, labda tunaweza kuzifananisha na studio za BBC, CNN au Al Jazeera.

“Tunataka kuhakikisha tunaleta mapinduzi ya utangazaji wa television nchini hasa katika suala la michezo, wapenzi wa michezo wategemee mambo makubwa kutoka kwetu,” alisema Mhando.

Azam TV imekua ikionesha moja kwa moja (live) mechi zote za ligi kuu Tanzania bara na wanatarajia kuboresha matangazo hayo ya mpira ili kuwapa burudani zaidi wapenzi wa michezo huo nchini na nchi zote ambako matangazo ya Azam TV yanafika.

No comments:

Post a Comment