KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 8 March 2015

WANAWAKE TUMIENI VIZURI FURSA ZA MITAJI

Mke wa Rais Salma Kikwete
MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete amewataka wanawake kutambua kuwa kujikwamua kwao kiuchumi kutaanza ndani ya nafsi zao wenyewe.
Sambamba na hilo, baadhi ya wanawake wa kawaida wamesema hawaitambui siku hiyo ya wanawake duniani.
Mama Kikwete alitoa kauli hiyo, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazimmoja jijini jana.
Alisema kujikwamua huko kutatokana na dhamira sahihi na ya dhati ya mhusika kuheshimu kila fursa anayoipata na kuanzia hapo atakuwa amejifungulia milango ya mafanikio.
“Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Risala yenu mmeongea masuala mbalimbali mazuri.
“Kuhusu changamoto ya mikopo yeneye riba nafuu, serikali kupitia Mfuko wa kuendeleza wanawake na Vijana inaendelea kutoa mikopo hiyo kupitia Halmashauri za Manispaa za Mkoa huu,”alisema Mama Salma.
Mama Kikwete alisema katika mwaka wa fedha  2014/15, Halmashauri zote tatu za mkoa huo zimetenga jumla ya sh bilioni 1.50 (1,050,000,000).
Alisema wilaya ya Ilala imetenga sh milioni 500, Kinondoni  sh. milioni 250 na Temeke sh milioni 300 .
Kutoka na fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya wanawake na vijana, anawashauri watumie fursa hiyo ya mikopo iliyopo katika ngazi ya halmashauri kujiletea maeneleo.
Katika kumkwamua mwanamke, itakumbukwa kuwa mwaka 2012 aliwahi kuzindua mpango kasi wa uwezeshaji wa wanawake na wasichana na Desemba 2014 alizindua mpango mwingine wa kuzuia mimba za utotoni.
Mama Salma, alisema lengo lilikuwa ni kuwawezesha wasichana kuendelea na masomo tangu elimu ya msingi hadi chuo kikuu.
Alitoa wito kwa wanawake kuendelea na juhudi za kujikomboa kielimu na kiuchumi kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali, kujiunga na vikundi vya kiuchumi vilivyoko katika maeneo yao kama vile vya VICOBA na vinginevyo vya kuweka na kukopa.
Aidha, Mama Kikwete, alisema wanawake wa mkoa huo wameendelea kukuathirika zaidi ikiwemo maradhi kama vile, Ukimwi, vifo vinavyotokana na uzazi ambavyo vinaweza kuzuilika.
Athari nyingine ni unyanyasaji wa kijinsia, kubakwa, mimba za utotoni na kunyimwa haki ya kumiliki mali hususan ardhi.
“Hivyo, basi maadhimisho hayo si kwa ajili ya kufanya sherehe tu, pia ni kufanya tathimini kwa pamoja kutafakari namna gani tumepiga hatua katika kukabiliana na changamoto hizo,”alisema Mama Kikwete.
 Alisema baada ya kutafakari wazijadili  na kutafuta mbinu na mikakati bora zaidi katika kumkomboa mwanamke na changamoto hizo. 
Wanawake wa Kawaida
Wanawake wa kawaida baadhi yao wamesema hawaitambui siku hiyo, wanachojua ni yawanawake wanaofanyakazi maofisini.
Tatu Daud ambaye ni mfanyabiashara ya kuuza vitafunwa eneo la Posta mpya alisema pamoja na kuwako viongozi wanawake lakini hawajajitokeza katika kukemea manyanyaso wanayofanyiwa na mgambo wa jiji kwa kukanyagakanyaga biashara zao.
Alisema serikali imewatenga, hawndewi haki wananyanyaswa, wanafukuzwa viumbe vyenye madhara kila wanapojaribu kutafuta kipato kwa siku hii ni ya maombolezo kwetu.
Hadija Mwalimu, alisema serikali inawashauri wakope mikopo ili wajikwamue kiuchumi lakini cha kushangaza serikali hiyo inawazuia wasifanye biashara katika maeneo ambayo yanawateja wao.
“Tunakamatwa na askari wa jiji na kwenda kulipishwa faini y ash 50,000 wakati hata mtaji tuliokopa ni sh 20,000 kweli utasema wanawake tunathaminiwa na ukiangalia fedha hizo ndio tunazitegemea kulisha familia na kupeleka watoto wetu shule na mambo mengine,”alisema Hadija.

No comments:

Post a Comment