KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 23 March 2015

LOWASSA AZIDI KUSHAWISHIWA AGOMBEE URAIS

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais. 

Lowassa, amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu. Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura.


Baadhi ya umati uliofika nyumbani hapo kwa Lowassa hii leo.

No comments:

Post a Comment