NA MWANDISHI WETU
Naye Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi akihutubia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya
Mbunguni amewaambia wananchi katika mkutano huo amemshutumu Waziri wa Maliasili
na Utalii Mh.
Lazaro Nyalandu kwa kutosikiliza ushauri alioutoa Katibu Mkuu wa
Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa wilayani Loliondo na
Ngorongoro kwa mawaziri ambao wizara zao zinahusika moja kwa moja katika maamuzi
na kushughulikia matatizo ya migogoro ya Ardhi mkoani Arusha ambapo kumekuwa na
migogoro karibu wilaya zote, kati ya mbuga za wanyama na vijiji ama kati ya
vijiji na vijiji.
Nape amesema wakati waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mh. William Lukuvi akiitikia na kupokea ushauri huo na kuhamishia
shughuli zake mkoani Arusha ambapo kwa sasa yuko mkoani humo akikutana na
viongozi mbalimbali pamoja na wananchi ili kutatua migogoro hiyo, Nyalandu
amekaa kimya anaendelea na mambo yake.
CCM ndiyo yenye mkataba na wananchi
kwani ndiyo iliyoomba kura kwa wananchi na Mh Waziri Nyalandu ana mkataba na
CCM ambayo imempa kazi ili afanye kazi na kutatua matatizo ya wananchi, CCM
haiwezi kukubali mambo yaiharibike kwa watendaji wa serikali kutowajibika kwa
wananchi kwani ndiyo itakayoadhibiwa na wananchi wakati wa uchaguzi ujao,
“Hivyo Nyalandu anatakiwa kufanya kazi ambayo CCM imempa na si kutafuta watu wa
kumtetea si sawa” Amesema Nape Nnauye.

No comments:
Post a Comment