KATIKA taarifa hiyo ya BRN, pamoja na mafanikio yaliyoonekana katika maeneo mengi ya kipaumbele, tatizo kubwa linabaki katika upande wa elimu, hasa masilahi na uwezeshaji wa walimu.
Ripoti hiyo inaeleza kwamba utafiti umeonyesha ni asilimia 27 hadi 39 tu ya walimu ndio walioridhika na mazingira yao ya kazi.
Tatizo kubwa linalowakera ni kucheleweshwa kwa malipo yao ambapo wana madai ya zaidi ya sh. bilioni 5.7 kutoka kwa mwajiri wao, yaani serikali.
Hata hivyo katika ripoti hiyo inaeleza kwamba serikali iko tayari kuhakikisha kwamba wanalipwa madai yao yote, na kwamba utaratibu mzuri unaandaliwa ili kuepuka matatizo ya aina hiyo.
Nishati
Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kwamba katika suala la nishati, kumekuwa na ongezeko kubwa ambapo katika mwaka 2013/14 kila mtumiaji alikuwa na uwezo wa kutumia kwh 105.8 ikilinganishwa na mwaka 2012/13 ambao uwezo ulikuwa kwh 97.
Hii ilitokana na kupunguzwa kwa mwanya wa kupotea kwa nishati kutoka asilimia 21 hadi 19. Pia umeme umewafikia watumiaji wapya 193,420.
Bajeti
Kuhusu bajeti, taarifa hiyo inaonyesha kwamba
serikali imeweza kufukia pengo la upungufu katika nakisi ya bajeti kufikia sh. trilioni 6.7 kutoka sh. trilioni 6.9. Hii ni hatua muhimu kufikiwa katika kipindi cha miaka mitano.
Matumizi yamepunguzwa kutoka asilimia 23.9 hadi asilimia 18.4.
Katika upande wa mapato, serikali imeongeza vyanzo vipya vya kodi vya zaidi ya sh.bilioni 455 na vyanzo visivyo vya kodi vilivyoingiza sh. bilioni 31.69.
Bandari
Kwa upande wa bandari, imeweza kuhudumia tani milioni 14.26 mwaka 2013/14 na kuvuka lengo la tani milioni 13.
Kilometa 127 za barabara zimejengwa kwa kiwango cha lami ikilinganishwa na kilometa
42 zilizotarajiwa kwa mwaka.
Maji
Miradi ya maji imewezesha watu wengi zaidi kupata maji katika mwaka mmoja.
Vituo 9452 vya maji vimejengwa na kuwapa fursa watu milioni 2.36 kwenye vijiji 240 kuwa na uhakika wa maji.
Lengo la awali la kuwafikia kati ya watu 300,000 hadi 500,000 limevukwa.
Kilimo
Eneo muhimu ambalo limewekewa mikakati ni kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yote yenye vyanzo vya maji ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula hasa mahindi namchele.
No comments:
Post a Comment