NA MWANDISHI WETU
JUMUIYA ya Wabaha’i jijini Dar es Salaam wanaungana na Wabaha’i wengine ulimwenguni kusherehekea mwaka wao mpya (Naw-Ruz).
Ofisa Mwenezi wa Baraza la Kiroho la Mahali Wabaha’i wa Dar es Salaam, Qudsiyeh Roy, alisema jana kuwa sherehe hizo zitafanyika Machi 21, mwaka huu, Baha’I Senta, iliyopo Mtaa wa Mfaume, Upanga, Dar es Salaam.
Alisema katika sherehe hizo kutakuwa na mkusanyiko wa ibada na kwamba sala za Kibaha’i zitasomwa katika lugha mbalimbali.
Naw-Ruz katika imani ya Baha’i ni mojawapo ya siku takatifu tisa kwa wafuasi wa imani hiyo ya Baha’i ulimwenguni kote na siku ya kwanza ya kalenda ya Baha’i.
Siku hiyo ya Naw-Ruz hufuata mwezi wa Kibaha’i wa mfungo. Mwaka wa Kibaha’i una miezi 19 na siku 19. Katika mwezi wa mfungo, Wabaha’i husali na kutafakari na hujitahidi kurekebisha tabia yao, kutakasa mioyo yao na kufikia daraja la juu zaidi la kujitenga na mambo ya dunia.
No comments:
Post a Comment