KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 1 March 2015

WASANII WAMLILIA KEPTEN KOMBA



BAADHI ya Wasanii wamesema wamepoteza kamu ya muziki kutokana na kifo cha Kepteni Komba, kilichotokea katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam juzi, kilichosababishwa maradhi ya kisukari..
Kauli hiyo ilitolewa na wasanii hao jana wakati walipokwenda nyumbani kwa marehemu Kepteni Komba Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kutoa pole kwa ndugu wa marehem.
Walisema hivyo, kwa vile Komba alikuwa msanii wa pekee ambaylikuwa na uwezo wa kutunga nyumbo za matukio pindi yanapotokea ghafla.
Ummy Wenceslaus (Dokii), alisema Kepteni Komba alikuwa mtu ambaye aliwasaidia wasanii wengi ambao baadhi yao walifanikiwa akiwemo Ramadhan Masanja (Banza Stone).
“Alikuwa ni mtu mwenyekipaji mwenye sauti nzuri na yapekee, alikuwa anasikiliza watu alikuwa akitoa ushauri kwa kila aliyekuwa akitaka kukamilisha malengo yake,”alisema Dokii.
Dokii, alisema wamepoteza mpiganaji wa kweli katika fani kwani alikuwa chapa kazi na kwamba alikuwa akijiamni katika maamuzi yake.
Naye Rais wa Shirikisho la Muziki wa Nyimbo za Injili, (Shimuta), Ado Novemba, alisema alikuwa mtu wa ajabu kwani kutokana na madaraka aliyokuwa nayo angekuwa kiongozi mwingine angeacha kupiga muziki lakini kwake ilikuwa tofauti.
Aidha, walisikitishwa na baadhi ya watu wanaotoa taarifa mbaya kuhusu marehemu, kwa kweli siyo vizuri, na watambue kuwa marehemu hana makosa.

No comments:

Post a Comment