KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 23 March 2015

WAZAZI MAGOLE WASHINIKIZA MWALIMU AONDOLEWE

WAZAZI wenye watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Magole, wilayani Ilala wameandamana wakiimshinikiza Ofisa Elimu wilaya hiyo Elizabeth Thomas, kumuondaoa Mwalimu Stella Mhando kutokana kushindwa kuunda kamati ya shule kwa miezi sita.

Naye Ofisa Elimu wa Wilaya, Elizabeth, amesema wanaomshinikiza  afanye hivyo ni watu ambao wanamuogopa mwalimu huyo ambaye ameweza kuwadhibiti katika mipango yao ya kutaka kupora eneo la ardhi la shule hiyo.

Akizungumza na wandishi wa habari leo, mmoja wa zazi hao, Rogers Msindo, alisema kushindwa kwake kuunda kamati hiyo kumesababisha wazazi wakose pakuwakilisha kero zinazojitokeza katika shule hiyo. 

Alisema walifikia hatua hiyo kwa vile kama watamuacha mwalimu huyo aendelee kwa mtindo huo kuna hatari wakashindwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao hata gundua vitendo vibaya vinavyofanywa na mwalimu huyo.

“Hivi sasa kuna kero mbalimbali za watoto kutofundishwa, michango isiyoeleweka huku pia kukiwa na madai mengine yote hayo tunashindwa kuyapatia ufumbuzi kutokana na kukosekana kamati hiyo ambayo pia ingemsaidia kujibu baadhi ya lawama zinazoelekezwa kwake,”alisema Msindo. 

Msindo, alisema hawamtaki mwalimu huyo na baadala yake wapelekewe mwingine wakisisitiza kuwa hawataki majadiliano ya aina yeyote isipokuwa utekelezaji wa agizo lao.

Ofisa  Elimu wa wilaya hiyo, Elizabeth Thomas, alisema hawawezi kumhamisha mwalimu huyo kwa vitu ambavyo wakati mwingine wao ndio kikwazo.

Alisema, madai ya wananchi hao hayana ukweli bali wanampinga mwalimu huyo kwa vile amekuwa kikwazo katika nia yao ovu iliyosababisha mgogoro mkubwa wa uporwaji wa eneo la ardhi, ya shule hiyo.

Elizabeth, alisema wanampiga vita ondoke, wakiamini kuondoka kwake kutawasaidia kupata urahisi wa kugawana eneo la ardhi ya shule hiyo hakari 20, ambalo mwalimu Stella analifahamu vizuri kuliko mgeni atakaye kuja. 

Hata hivyo, alisema mchakato wa kupatikana Kamati hiyo umekamilika na wananchi hao wanajua kuwa hadi Alhamis, Kamati hiyo itakuwa imepatikana.


Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa Magole, Lucas Chacha, alikiri kuwa wananchi hao, waliandamana, huku akiwataka kuwa watulivu kwa vile amekutana na Uongozi wa shule na kwamba wamekubaliana kuwa kesho kamati hiyo itachaguliwa.

No comments:

Post a Comment