KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 19 March 2015

ZAIDI YA WATOTO 10,000 WANASHAMBULIWA NA SIKO SELI

Mtoto Nira Khamis (12), anayesumbuliwa na ugonjwa wa ‘siko seli,’ akionyesha simu aina ya ZTE ambayo atatumia kwa ajili ya kujirekodi na kutuma video wakati akimeza dawa. Jumla ya simu 150 zimetolewa msaada na Vodacom Foundation katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli, kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Reenu Verma na kulia ni Mratibu wa matibabu kwa njia ya teknolojia, Dk. Deogratius Soka. (Na Mpiga picha Wetu).

NAMWANDISHI WETU

WATOTO 11,000 hulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kila mwaka kutokana na kushambuliwa na ugonjwa upungufu wa damu mwilini (Siko Seli).
 Mratibu wa Kitengo cha Siko Seli, Dk Robert Mongi, alisema hayo wakati akipokea msaada wa simu 150 za mkononi kwa ajili ya  kuratibu matibabu ya wagonjwa wanaotibiwa kwenye kitengo hicho.
 Simu hizo zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya  jamii ya Vodacom Foundation.
 Alisema tatizo la ugonjwa huo kwa watoto ni kubwa nchini na limekuwa likiongezeka kila mwaka na kusababisha watoto wengi kulazwa.
Hata hivyo, Dk. Mongi alisema ugonjwa huo  unatibika iwapo mgonjwa atapima na kuanza kutumia dawa mapema ikiwemo kuzingatia
“Vipimo vya ugonjwa huo vinapatikana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tu, hali ambayo inasababisha waathirika wa ugonjwa huu wanaoishi nje ya mkoa wa Dar es Salaam kuchelewa kupata vipimo na wengi wao kupoteza maisha,”alisema Dk. Mongi.
Alisema kutokuwepo mashine za kupima ugonjwa huo za kutosha ni moja ya changamoto kubwa inayokwamisha kuutokomeza ugonjwa huo nchini.
  Aidha,  Dk. Mongi aliishukuru Vodacom Foundation kwa msaada huo ambao utawafikia walengwa hususan wagonjwa wanaotumia dawa pia zitwasaidia katika huduma nyingine muhimu kiafya.
Meneja wa Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza alisema kampuni ya Vodacom kupitia taasisi yake hiyo imeona kuna  umuhimu wa kuwapatia wagonjwa simu ili ziwasaidie wakati wa matibabu yao.
 “Tunajua kuwa kuna makundi mengi ya wahitaji katika jamii hivyo tumeona safari hii tuangalie kundi la wagonjwa  wanaotibiwa Siko Seli kwa kuwa ugonjwa huu unazidi kuongezeka na unahitaji jitihada za ziada kutoka kwa wadau mbalimbali katika kuutokomeza”.Alisema Rwehikiza.

No comments:

Post a Comment