![]() |
| Askofu, Pengo |
ASKOFU
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam,
Mwadhama Polycarp Karidinal Pengo, amesema mashambulizi ya yaliyofanywa na
kikundi cha kigaidi cha Al Shabab katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya yamewatia
hofu Wakristo.
Askofu Pengo alisema hayo wakati ibada ya misa
takatifu iliyofanyika katika Palokia ya kipawa na kuwakutanisha wanakwaya wa
kanisa hilo
jijini Dar es Salaam leo.
Alisema,
mauaji ya baadhi ya wakristro yaliyotokea katika Chuo Kikuu cha Garissa, hakuna
mtu aliyeamini kwamba vikundi hivyo vibaya vingevamia na kuanza kuwauwa wakristu.
Askofu
Pengo, alisema jambo hilo limewatia hofu na
wasiwasi mkubwa kwani hawakuwahi kufikiria hata siku moja kama vitendo
hivyo vya kigaidi vingeweza kutokea.
“Nawaomba
niwaulize hivyi nani aliamini kuwa Kenya
wangeweza kuvamiwa tena na kikundi cha kuvunja amani na kuchagua wakristo na
waislamu kisha kuwauwa wakristo, hali hii inatisha sana
na kusikitisha kama sasa wanaanza kuuwawa watu kutokana na dini
zao,” alisema.
Askofu
Pengo alisema zamani vita ya watu wa Kenya
ilikuwa makabila kwa makabila lakini
sasa imekuwa tofauti imeingia katika dini hivyo wakristu wanauwawa pasipo na
hatia katika nchi yao.
“Tulijua
kuwa Kenya wanagombana kwa
makabila lakini kwamba wataanza kuulizwa wewe ni mkristu unapigwa risasi ila mwiislamu
anachwa huru, hili ni jambo la hatari inatubidi kumuomba sana
mwenyezi Mungu atuepushe na balaa hilo
lakini pia tuiombee nchi ya
Kenya iwe na amani,” alisema.
Hata
hivyo Askofu Pengo aliwataka waamini wa kikristo kuwa na ujasiri wa kubaiki na
msimamo kwa kutoiga dini ya wengine kwa kuogopa kuuliwa na kumuommba mungu
awaimarishe na kudumu kwenye imani yao huku wakikumbuka utukufu wa Bwana Yesu.

No comments:
Post a Comment