KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 9 April 2015

Basi la Ngorika likiwa halitamaniki baada ya kugongana uso kwa uso la basi lingine la Kampuni ya RATCO katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye eneo la Kijiji cha Mbweni, Mkata mkoani Tanga. kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio,inadaiwa kwamba mpaka sasa ni Watu kumi wamepoteza maisha katika ajali hiyo, akiwepo Dereva wa Basi la Ratco.Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mpaka sasa. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga kwa maelezo zaidi.(KWA HISANI YA MICHUZIBLOG)


 Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment