KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 9 April 2015

MAHAKAMA YA WILAYA DODOMA YA AHIRISHA KESI YA MINJA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Minja
MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imeahirisha kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja hadi Mei 7 mwaka huu  kutokana na upande wa serikali kutokamilisha uandaaji wa maelezo ya awali.

Ombi la kuahirishwa kesi hiyo lilitolewa jana na Wakili wa Serikali, Rose Shio, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo.

Baada ya kuwasilishwa kwa ombi hilo, Wakili wa mshtakiwa, Godfrey Wasonga, alisema hana pingamizi, hivyo Hakimu Mfawidhi, Rhada Ngimilanga kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 7 mwaka huu.
Minja ambaye yupo nje kwa dhamana, katika kesi hiyo anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuwachochea wafanyabiashara kutenda kosa na kuwazuia kulipa kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki za (EFD’s).


No comments:

Post a Comment