KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 13 April 2015

CHAMA CHA KIJAMII NA UZALENDO CHAPATA USAJILI WA MUDA

 Kulia ni MSAJILIWA Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza akimkabidhi Mwenyekiti wa CKUT, Ramadhan Semtawaa cheti cha usajili wa muda.

SAJILIWA Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza amesema chama cha siasa ili kifanye vizuri kinahitaji kuwa na misingi ya utawala bora, baadae kifikie malengo yake ya kushika dola.

Miongoni mwa misingi hiyo ni pamoja na kuwa na Katiba yenye misingi ya kidemokrasia.  

Nyahoza, alisema hayo, jijini leo wakati akikabidhi cheti cha usajili wa muda kwa Mwenyekiti wa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (C.K.U.T), Ramadhan Semtawa.

Alisema, kila chama kina hitajika kujenga demokrasia ya kweli ambayo ni muhimu hususan ikaanza ndani ya chama kwani itawasaidia viongozi  kufikia malengo waliyojiwekea.

Nyahoza, alisema viongozi pia wanawajibu wa kusoma sheria ya vyama vya sisasa ili kuepuka migongano na watendaji wa taasisi zingine za serikali.

“Leo tumetoa cheti cha usajili wa muda kwa chama cha CKUT, tunawaomba sana viongozi wa chama hiki kukaa pamoja na wanachama wenu ili kupeana mawazo mazuri ya kujenga chama.

“Asitokee mmoja miongoni mwenu akadai kuwa yeye ndiye mwenye chama, nawashauri someni vizuri sheria ya vyama ili kuepuka mgogoro na taasisi zingine,” alisema.
Naye Msajili wa Vyama vya Siasa, Mstaafu Jaji Francis Mutungi, alisema ofisi ya msajili ni taasisi maalum na iko pale kwa ajli ya kuwahudumia watu wote wanaohitaji huduma kama hiyo.

Mwenyekiti wa chama hicho cha CKUT Semtawa, alisema wameanzisha chama kwa malengo maalumu ya kurejesha nchi kwenye misingi ya waasisi ambao walijali haki za wanyonge.

Alisema, nchi imetawaliwa na rushwa kila kona jambo ambalo limewafanya wananchi wanyonge wakose haki zao.

Semtawa, alisema kutokana mazingira hayo CKUT, kitakapoingia madarakani kitahakikisha kuwa kina rudisha nchi katika misingi ya kidemokrasia na utawala bora.
“Watu wanauwa kwa sababu za kidini na wengine upoteza maisha yao kwa imani za kishirikina, lakini pia wapo watu wamekuwa wakila fedha za serikali na hawachukuliwi hatua yoyote, tunataka kuja kuibadilisha nchi hii maana aina muelekea kwa sasa,” alisema.
Semtawa alisema kazi kubwa iliyoko mbele yao ni kutafuta wanachama ili waweze kupata usajili wa kudumu jambo ambalo anaamini kuwa litafanikiwa.

“Tunatakiwa tuwe na wanachama 2000 katika mikoa kumi na kila mkoa mmoja inatubidi tupate wanachama 200, tumejipanga vizuri na tunaamini kuwa tutapata usajili wa kudumu,”alisema.

Aidha, Semtawa alisema hawatahitaji kiongozi yoyote kutoka katika vyama vya upinzani kujiunga na chama hicho kwa vile kufanya hivyo kutapunguza nguvu ya upinzani.

Alisema chama hicho kiko tayari kupokea viongozi wasafi kutoka CCM, ambao hawakubaliani na vitendo vichafu vinavyofanywa na wenzao wasiozingatia maadili ndani ya chama hicho.

“Hatutawapokea tu bali tutawachunguza kwanza mienendo yao tangu wakiwa ndani ya chama hicho na hata uadilifu wao nje ya chama,”alisema Semtawa.



No comments:

Post a Comment